 |
Katibu wa siasa na uenezi wa CCM Wilaya ya Geita,Bw Jonathan
Masele pamoja na baadhi ya viongozi wakishiriki kuchimba msingi kwenye shule ya msingi ya Kaseni iliyopo Kata ya Mtakuja. |
 |
Viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM)wakishiriki kuchimba msingi wa shule ya msingi Kaseni. |
 |
Kaimu afisa elimu halmashauri ya mji wa Geita,Mwl
Salome Cheleani,akishiriki zoezi la uchimbaji wa msingi wa shule ya msingi Kaseni. |
 |
Mwenyekiti wa CCM wilayani ya Geita ,Barnabas Mapande akishirki zoezi la uchimbaji wa msingi shule ya msingi Kaseni. |
 |
Wananchi wakiwa kwenye zoezi la kuchimba msingi shule ya msingi Kaseni. |
 |
Wananchi wakiwa wamesimama mbele ya msingi wa shule ya msingi Kaseni. |
 |
Katibu wa siasa na uenezi wa CCM Wilaya ya Geita,Bw Jonathan Masele akizungumza na waandishi wa habari juu ya kujitolea katika shughuli ya ujenzi wa madarasa. |
 |
Wananchi wakisomba mawe kwaajili ya ujenzi wa msingi wa shule ya Kaseni.
Na,Joel Maduka,Geita
Halmashauri
ya mji wa Geita inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa elfu moja na
sabini na tisa (1,079) huku mahitaji yakiwa ni elfu moja miatano na
saba (1,507) na ambavyo vipo ni mianne ishirini na nane (428) .
|
Hali hii
imewasukuma viongozi wa Chama cha
mapinduzi (CCM) Wilayani Geita,kushirikiana na wananchi kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya
msingi Kaseni iliyopo Kata ya Mtakuja
Wilayani humo,lengo likiwa ni kupunguza changamoto ambazo zimeendelea kuwakumba wanafunzi kusomea nje.
Akizungumza
wakati wa shughuli hizo ,Katibu wa siasa na uenezi wa CCM,Bw Jonathan Masele
amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na ilani ya chama kuelekeza kushiriki
katika suala la maendeleo na kwamba kufanya hivyo kutasaidia kuwaepusha watoto kukaa nje ya madarasa.
“Tumeamua kwa sababu ilani yetu ya chama cha mapinduzi
inaelekeza kutekeleza majukumu ya wananchi kwa kuwasaidia kujenga mashule
kufanya kazi za mikono ,hii ilani yetu tunaitekeleza ili kuhakikisha watoto
wanasoma kwenye mazingira mazuri”Alisema Masele.
Mwenyekiti
wa CCM wilayani humo,Barnabas Mapande amewataka wananchi kujitolea kufanya kazi
za maendeleo na kuachana na dhana ya maandamano yasiyokuwa na msingi kwa Taifa
,kwani ni vyema kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais za kuboresha miundombinu
ya Elimu.
“Tunahitaji
kufanya kazi muda wa maneno umekwisha awamu hii ni ya kazi wanaosema maandamano
wakaandamane lakini hutakiwi kuandamana kama unataka maandamano kasombe mawe,
kuchimba msingi tufanye kazi kwa ajili ya watoto wetu wanaandamana waende huko
lakini cha moto watakiona sisi tufanye kazi za maendeleo”Alisisitiza Mapande.
Aidha Kaimu
afisa elimu halmashauri ya mji wa Geita,Mwl Salome Cheleani ameelezea kuwa
wanaendelea na mikakati ya ujenzi wa madarasa na kuyamalizia maboma ambayo
yalikuwa bado hayajakamilika na kwamba wana imani mwaka huu watapunguza kwa
kiasi kikubwa mahitaji ya vyumba vya madarasa.
Post A Comment: