![]() |
Msimamizi wa Mradi wa Shirika la maendeleo la nchini Uholanzi (SNV) Bw,Jackson Wandera akizungumza na wadau wa sekta ya afya juu ya mradi ambao ulikuwa umelenga kuimiza matumizi sahihi ya vyoo. |
Halmashauri ya wilaya ya Geita imeibuka kidedea katika
matumizi safi ya vyoo dhidi ya wilaya za Babati, Karatu, Chato na Kwimba zilizoshiriki katika mradi wa Usafi wa mazingira
endelevu kwa watu wote uliokuwa ukisimamiwa na Shirika la maendeleo la nchini Uholanzi (SNV).
Hayo yameelezwa na Jackson Wandera wakati wa kikao cha
wadau cha kufunga mradi na kuweka
mikakati ya kundeleza programu hiyo ulioshirikisha
vijiji 72 kwa muda wa miaka minne kuanzia mwaka 2014 hadi machi 31 mwaka huu
kwa vijiji ambavyo vilikua havipo katika Mpango wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi
wa Mazingira(NSC).
“Mwaka 2014 hali ya uchafu wa mazingira ilikua mbaya
kutokana na kukosa vyoo safi na bora kwa
wakazi wa Geita, ambapo asilimia 24% ya wakazi
wa vijiji hivyo 72 walikua wanajisaida vichakani. Asilimia 65% walikua
na vyoo vya kawaida, Asilimia 38% walikua na vyoo bora na asilimia 1% tu ndio walikua wananawa mikono yao baada ya kutoka chooni
hali iliyopelekea mlipuko wa magonjwa
kama kipindupindu na hii ni sababu kubwa iliyotufanya SNV kuungana nanyi
kusaidia jamii ya Geita.” Alisema Wandera
Aidha Wandera ametoa matokeo ya tathimini na kuisifu
Halmashauri kupiga hatua na kuondoa tatizo la kujisaidia porini kwa kufikia
asilimia 01%ukilinganisha na wakati mradi huu unazinduliwa, Pia wakazi
wanaotumia vyoo wamefikia asilimia 95%,wale wenye vyoo bora wamefikia asilimia
87% na wakazi wanaonawa mikono na sabuni
baada ya kutoka chooni ni
asilimia 04%.
Kwa upande wa mwakilishi kutoka Idara ya elimu Msingi
Mwalimu Nassuna Henry alisema tayari elimu ya matumizi safi na bora ya vyoo
imefika katika shule zote za msingi 176 na inasisitizwa kutumia vyoo vya safi
vinavyosaidia kulinda mazingira na kwa gharama nafuu.
Mradi huo ulishirikisha wilaya za Chato, Geita, Kwimba,
Babati na Karatu kwa lengo la kusaidia jamii kuimarisha matumizi bora ya vyoo, Kunawa mikono na
sabuni baada ya kutoka chooni na kusisitiza matumizi ya vyoo bora vya safi
ambavyo ni vya bei nafuu.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Washirika wa maendeleo kutoka shirika la SNV,
Watendaji wa Kata, wadau wa SNV vijijini pamoja na waandishi wa habari.
Post A Comment: