Meza kuu ikiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali na chama cha mapinduzi.
Na,Consolata
Evarist,Geita
Baraza la
madiwani wa halmashauri ya mji wa Geita,Wilayani Halmashauri ya Mji Geita limepitisha makadirio ya bajeti ya matumizi
ya ya mwaka wa fedha 2018/2019 kiasi cha shilingi Bilioni 44,983,764,197.00
katika shughuli mbalimbali za Halmashauri. Kati ya Fedha hizo Jumla ya Tsh 15,585,248,344.00 ni kwa ajili ya shughuli za
Maendeleo ikiwa ni Mapato ya Ndani, Ruzuku ya Serikali na Wahisani mbalimbali. Tshs. 4,765,976,688.00 kwa ajili ya matumizi
ya kawaida ikiwa ni Ruzuku kutoka Serikali kuu na Mapato ya ndani na Tshs.
24,632, 539,165.00 kwa ajili ya mishahara.
Aidha
Halmashauri imekisia kukusanya Jumla ya
Tsh 5,114,157,735.00 toka vyanzo vya ndani ambayo fedha hii imejumuishwa
katika jumla ya Bajeti ya mwaka
2018/2019. Jumla ya Tsh. 3,030,016,641.00 sawa na 60% zimetengwa kwa ajili ya
Miradi ya Maendeleo.
Akiongeza katika
ukumbi wa Halmashauri ya Mji Geita kwenye kikoa cha kupitisha
bajeti ya Mwaka wa fedha 2018/2019,Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest
Aporinali alisema Bajeti hyo imezingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye
Mwongozo wa kuandaa Bajeti uliotolewa na Wizara ya Fedha Mwezi, Novemba 2016,
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs 2030); Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015-2020, Mpango wa Pili wa miaka Mitano (FDYPII) 2016/17-2020/21 na Lengo likiwa ni kufikia Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2030.
“Mpango na Bajeti kwa
Mwaka wa Fedha 2018/2019,kwenye
halmashauri hiyo kuwa imejielekeza katika kufikia vipaumbele vyenye
shabaha na malengo yafuatayo Kuendelea
kuboresha na kuimarisha mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani ili kuongeza
mapato ya Halmashauri. Kuboresha Sekta za huduma za jamii, hususan, Elimu, Afya, Maji, Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo,
Misitu, Maendeleo ya Jamii, Ushirika.Kusaidi Sera ya Taifa kufikia Uchumi wa
kati wa uendelezaji wa viwanda.Kuimarisha Utawala bora”Alisema Modest
Aidha ameongeza kuwa Halmashauri inategemea
kukusanya mapato yake kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama kodi ya huduma(
service levy) kutoka kampuni ya Mgodi wa Dhahabu Geita na Kampuni nyingine
zinazofanya kazi na Mgodi huo, kodi ya nyumba za kulala wageni, Leseni za
biashara,faini mbalimbali, upigaji chapa mifugo na ushuru wa mifugo, ushuru wa
mazao mbalimbali na matunda.
“Katika Bajeti ya mwaka
2018/2019. Jumla ya Shilingi 15,585,248,344 zimetengwa kwa ajili
ya Miradi ya Maendeleo, Kiasi cha shilingi 24,632,539,165 kwa ajili ya
mishahara ya watumishi na Shilingi 4,765,976,688 kwa ajili ya matumizi
mengineyo”. Aliongeza Mhandisi Aporinaly
Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Mji Geita Mheshimiwa Leonard Kiganga Bugomola alisema kwa mwaka wa fedha uliopita Halmashauri
ilipanga kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 5, ambapo hadi kufikia mwezi
Disemba 2017 Halmashauri imeweza kukusanya kiasi cha Shilingi 2,868,353,850.15
sawa na asilimia 52.
Mh. Bugomola ameongeza
kuwa kutokana na mafanikio ya ukusanyaji uliofikia nusu ya makadirio ana imani
kuwa mpaka kukamilisha mwaka wa fedha 2017/2018 mwezi Juni mwaka huu,
Halmashauri itakuwa imefikisha lengo la makusanyo. Aidha makusanyo hayo
yanatoa mwanga wa mafanikio katika bajeti iliyopitishwa kwa mwaka wa fedha
2018/2019.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi
amewasisitiza wajumbe kuwa na ukusanyaji mzuri wa mapato hili kuweza
kutekeleza bajeti kwa uzuri zaidi.
Katika Mpango na Bajeti
kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Halmashauri ya Mji Geita imejielekeza katika
kufikia vipaumbele vyenye shabaha na malengo ambayo ni Kuendelea kuboresha na
kuimarisha mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani ili kuongeza mapato ya
Halmashauri, Kuboresha Sekta za huduma za jamii, hususan, Elimu, Afya, Maji,
Barabara, Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Misitu, Maendeleo ya Jamii, Ushirika,
Kusaidia Sera ya Taifa
kufikia Uchumi wa kati wa uendelezaji wa viwanda na Kuimarisha Utawala
bora.
|
Post A Comment: