![]() |
Barabara inayotoka amerikani Chips Kuelekea Jimboni ikiwa kwenye hatua za awali za ujenzi. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza suala la mkandarasi kushindwa kutekeleza ujenzi wa Barabara kwa wakati. |
![]() |
Baadhi ya maeneo ambayo wananchi wameendelea kulalamika kuathiriwa na mvua kutokana na kifusi ambacho kimewekwa na mkandarasi kwenye Barabara ya Amerikani Chips inayoenda Jimboni. |
![]() |
Bi,Getruda Daud ambaye ni mkazi wa Katundu akilalamika namna ambavyo wameendelea kupata shida kutokana na kushindwa kukamilika kwa ujenzi wa Barabara pamoja na daraja. |
![]() |
Baadhi ya wananchi wakiangaika kuvuka kwenye kidaraja kidogo kutokana na kushindwa kukamilika kwa Daraja. |
![]() |
Nyumba ikiwa imeenea maji kutokana na kifusi ambacho kimelalamikiwa na wananchi.
Na,Joel Maduka,Geita
|
Wananchi
waishio Mtaa wa Katundu Kata ya Kalangalala Mkoani Geita wamemlalamikia
mkandarasi ambaye anajenga Barabara ya Kilomita 1.2 inayotoka Amerikani Chips
kuelekea Jimboni kuweka kifusi cha mchanga hali ambayo imekuwa ikisababisha
maji kuelekea kwenye makazi yao pindi mvua zinaponyesha.
Mkandarasi
huyo ambaye anajulikana kwa jina la Nyakiling’ani Constraction Limited(NCL) anatekeleza mradi
huo kwa ufadhili wa Benki ya dunia na
kusimamiwa na halmashauri ya Mji wa Geita.
Akizungumza
na Mtandao huu,Bi,Getruda Daudi alisema wameendelea kupata shida kubwa kutokana
na mkandarasi huyo kuweka kifusi na pindi wanapomwambia amekuwa akiwaambia hana
gharama za kukitoa kifusi hicho.
“Mvua
zikinyesha tumekuwa tukipata shida sanaa jamani yani maji yote yanakuja kwenye
nyumba zetu na sababu ni hiki kifusi ambacho mkandarasi amegoma kukitoa
tumekwisha mwambia hadi na diwani wetu lakini alikuja akapiga picha akaondoka
na sisi ndio tunaopata shida ila tunaona yuko kimya hatujui tufanyeje”Alisema
Bi ,Getruda.
Hata hivyo
kwa upande wake Bw, Nzugila
Mazoya pia amelalamika kitendo cha
mkandarasi wa eneo hilo kuchukua muda mrefu bila ya kukamilisha ujenzi wa
barabara hiyo pamoja na daraja hali ambayo kwa sasa imekuwa ikiwapa shida kwa
kuzunguka umbali mrefu kutokana na njia kuzibwa.
Sanjari na
hayo baadhi ya wafanyakazi ambao wanafanyakazi na Kampuni hiyo akiwemo
Lanslaus
Joseph na Majura Mfungo wamelalamikia
kutokulipwa mishahara kwa muda mrefu sasa na pindi wanapomuuliza msimamizi
amekuwa akiwasisitiza kufanya kazi kwa madai kuwa pesa itakuja na kwamba hawaoni
jitihada ambazo zinafanyika za malipo hadi sasa.
Kutokana na madai hayo
, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Mji kuhakikisha anaisimamia Kampuni ya Nyakiling’ani ikiwa ni
pamoja na kukatwa fedha kutokana na wananchi ambao wanaishi mitaa ya Katundu
kujitolea kuondoa kifusi hicho.
“Mtaro umejengwa mwaka
umefika kifusi kile kimekuwa ni mlima na kero kwa wananchi ,wananchi wale
wanakwenda kuondoa kifusi hicho sasa ni wito wangu mkateni huyo mkandarasi
maana ni ndani ya mkataba wake”Alisema Luhumbi.
Mkurugenzi wa halmashauri
ya Mji mhandisi Modest Apolinary alisema
amebaini kuwa kampuni hiyo ina uwezo mdogo wa kutekeleza mradi na
kwamba imewekwa kwenye uangalizi baada ya muda wa utekelezaji kuisha.
Kufuatia Malalamiko
hayo ya wananchi msemaji wa kampuni hiyo Bw, Raulent Mwita kwa Njia ya simu ambapo ameeleza
kuwa waliweka tuta kifusi hicho kutokana na ujenzi ambao wanaendelea nao kwa
sasa na suala la mvua namna lilivyokuwa likikwamisha ujenzi.
Post A Comment: