![]() |
Maandamano ya wanawake wakielekea katika dhifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe. |
Baadhi ya wakina mama wakionesha mabango ambayo walikuwa wamebeba wakati wa maandamano mbele ya mgeni Rasmi. |
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake,akikagua baadhi ya bidhaa ambazo zimetengenezwa na wakina mama wajasiriamali. |
Ni miaka 73
tangu Umoja wa Mataifa (UN), kupitisha maazimio ya tarehe ya leo kila mwaka
kuwa siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake kwa lengo la kupaza sauti zao juu
ya ukandamizaji na ukatili ambao umewafanya washindwe kushiriki maendeleo
endelevu ya familia na taifa kwa ujumla.
Chimbuko la
Siku ya Wanawake Duniani lilianza miaka mingi na mwaka 1911, baada ya Wanawake nchini
Marekani kuandamana kudai haki zao ambazo walikuwa wakizikosa: kama vile
kulipwa ujira mdogo, kufanyishwa kazi ngumu na kwa masaa mengi, kukosekana kwa
huduma za jamii na ubaguzi wa kijinsia.
Kila mwaka
maadhimisho haya yanafanyika na kubainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili
wanawake na kuwa kikwazo kikubwa cha kusonga mbele katika kujikwamua kiuchumi,
kiutamaduni na kisiasa.
Mkoani Geita
maadhimisho haya yamefanyika wilayani Bukombe,huku yakiuzuliwa na viongozi
mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo Mhandisi , Robert Luhumbi
pamoja na Naibu waziri wa madini ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo Doto
Biteko.
Mkuu wa mkoa
huo ambaye alikuwa ni mgeni rasimi ametumia nafasi hiyo kuvitaka vyombo vya habari kuendelea kuibua na
kutangaza vitendo vya ukatili ambavyo
vimekuwa vikifanywa dhidi ya wanawake na
watoto ndani ya jamii.
“Vyombo vya
habari wakiwa ndio wadau wakuu wa kuibua masuala mbali mbali yasiyo ya haki
ndani ya jamii ,kwa kushirikiana na serikali na jamii yote ,ushirikiano wenu wa
dhati wa kusaidia kuibua vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ndani ya
jamii,una umuhimu mkubwa .Pia niwasihi Jeshi la polisi ,kuimarisha madawati ya
jisnia na watoto kwenye vituo vya Polisi na kushirikiana kikamilifu na wadau wa
harakati za kuwakomboa wanawake na watoto kwa ajili ya kusaidia kupokea
,kufuatilia na kushughulikia kesi za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa
uharaka zaidi”alisema Luhumbi.
Akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Wilayani humo,Bi
Leticia Mourice alisema maendeleo ya wanawake katika Nyanja mbali mbali hapa
nchini ,yamekuwa yakikwamishwa na nafasi ambazo wanazo wanawake kama wazazi
walezi na wafanyakazi.
“Kwa upande
mwingine ,mila na desturi kandamizi kwa baadhi ya maeneo ,zimeendelea kujengwa
na kukuzwa.Jambo hili limeleteleza kutokuwepo na usawa kwa Jinsia katika Sekta
zote za maendeleo hususani katika Nyanja ya elimu,ajira,afya,umiliki wa
rasilimali ardhi,urithi na ushirikishwaji katika ngazi mbali mbali za maamuzi”Alisema
Bi,Leticia,
Siku ya
wanawake Duniani imepambwa na kauli mbiu isemayo” Kuelekea uchumi wa viwanda,
tuimalishe usawa wa jinsia na uwezeshaji
wa wanawake vijijini"
Post A Comment: