Wajumbe wa mkutano ambao ulikuwa umelenga kutoa ufafanuzi juu ya asilimi 10 ambazo zinatolewa na halmashauri kwa wanawake,vijana pamoja na walemavu Wilayani Geita. |
Katibu wa UWT,Bi Mazoea Salum akielezea akisoma mapendekezo ambayo wameyaadhimia kwenye Kikao hicho. |
Katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) Wilaya ya Geita,Julius Peter Akizungumza na wajumbe kwenye mkutano huo. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye Kongamano hilo akisisitiza suala la uanzishwaji wa viwanda vidogo kwenye vikundi. |
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Geita,Manjale Magambo akielezea umuhimu wa fedha asilimia 10 ambazo zimekuwa zikitolewa na halmashauri kwa vikundi vya vijana ,wanawake na walemavu. |
Na,Consolatha Evarist ,Geita
Kundi la watu wenye ulemavu kwenye halmashauri ya
mji wa Geita , wamelalamika kutonufaika na mkopo wa asilimia 2 kutoka
kwenye asilimia 10 ya Mkopo ambao umekuwa ukitolewa kwa wanawake na
vijana kutoka kwenye halmashauri hiyo hali ambayo imekuwa ikisababisha
kuendelea kuwa na maisha magumu pamoja na kuendelea kuunda vikundi
vya ujasiriamali.
Hayo yamebainishwa wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) , jumuiya ya wanawake(UWT) na
walemavu Wilayani Geita,kwa lengo la kujua namna ambavyo makundi
hayo yanaweza kunufaika na asilimia 10 ambazo zinatolewa na halmashauri kupitia
idara ya maendeleo.
Bw,Mathayo Peter akizungumza kwa niaba ya wenzake ambao wana ulemavu
alisema tangu kuanza kwa mpango huo ni
vikundi viwili tu vimekwisha kopeshwa pamoja na kuwa na vikundi vingi na hata
wakiulizia juu ya mikopo hiyo wamekuwa wakikutana na majibu ya kuwakatisha tamaa.
“Hii asilimia mbili ilikuwa ni nzuri tatizo linakuja kwenye idara ya
maendeleo ya halmashauri ya mji wa Geita kuwepo kwa baadhi ya watumishi kuwa na
kauli mbaya dhidi yetu kwani sijui huwa wanatuona hatuwezi lakini mimi niseme
na sisi tunaweza kwanza ukizingatia tunazo familia zinatutegemea kwanini wawe
wagumu kutupa hiyo mikopo”Alisema Peter.
Aidha kwa upande wake Katibu wa UWT wilayani humo,Bi Mazoea Salum amekiri
Kukosekana kwa uwelewa juu ya utoaji wa mikopo kwa vijana ,wanawake na walemavu
pamoja na kuwepo kwa urasimu ametaja kuwa ni kikwazo kwa walengwa wa mikopo
hiyo kwenye halmashauri ya mji wa Geita hali inayosababisha vikundi vingi
kusambaratika.
Mwenyekiti wa
uvccm wilaya Geita Manjale Magambo amewaomba viongozi kusimamia fedha hizo na
kutenda haki katika utoaji wa mikopo hiyo ili iweze kuwanufaisha walengwa na
kuweza kufikia azma ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake afisa
maendeleo ya jamii,Bi Valeria Makonda amesema kuwa kundi la watu wenye ulemavu
wanalitambua na kwamba hadi sasa wameshatoa mkopo kwenye vikundi viwili na
kwamba wataendelea kutoa kutokana na taratibu zilizopo.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi alifafanua kuwa
kutokana na uelewa wa elimu juu ya fedha ambazo zinatolewa na halmashauri ni
vyema wahusika wakawa na elimu ya kutosha ya kutambua ni namna gani wanaweza
kuzitumia fedha hizo.
Post A Comment: