![]() |
Baadhi ya Viongozi wa Kikristo mkoani Geita wamewataka
Wakristo kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa amani na utulivu na kujiepusha na
matendo maovu wakati wa sherehe hizo.
Padri Gerald Singu ambaye ni Paroko wa Parokia ya Bikra
Maria wa Fatima Geita, Mchungaji Gerson Yoboka ambaye ni kiongozi mkuu wa
kanisa Anglikana mkoani Geita na Mchungaji Mathias Michael Kasente wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri, KKKT Usharika wa Upendo wametoa kauli hiyo walipokuwa
wakitoa ujumbe wao wa Pasaka kwa Waamini.
Wamesema ni vema Wakristo wakabadilika na kuacha dhambi
badala yake wafanye mambo ya kumpendeza Mungu na kwamba baadhi ya watu wamekuwa
wakipania kufanya matendo maovu katika Sikukuu mbalimbali.
|
Navigation
Post A Comment: