![]() |
Dawa za kuuwa wadudu wa Pamba. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mkoa. |
Baadhi ya wakuu wa idara na wakurugenzi wakiwa kwenye Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwasisitiza wakurugenzi na wakuu wa idara mbali mbali kufanya kazi kwa Weledi.
Na,Joel Maduka,Geita.
|
Serikali mkoani Geita imekamata dawa za viuadudu 428
vilivyotakiwa kupelekwa kwa wakulima wa pamba vijijini badala yake vikapelekwa
kwenye maduka ya kilimo kinyume na matarajio ya serikali.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu wadau wa zao
la pamba walipokutana kujadili kilimo hicho.
Akizungumza na wakurugenzi na wakuu wa idara wa halmashauri
za mkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Luhumbi alisema hadi sasa
wanawashikilia watuhumiwa 12 wanaotoka kwenye halmashauri za Chato , Geita DC na Geita mji.
“Tumegundua viuadudu mia nne ishirini na nane(428)
vilivyotakiwa viingie vijijini kwa wakulima vimeingia kwa mawakala kwenye
maduka ya pembejeo kinyume na taratibu, mwongozo na mpango uliokusudiwa kwa hiyo watuhumiwa 12 tayari
wamekamatwa katika Wilaya mbili, wilaya ya Chato tumepata viuadudu tisini na
sita(96), Geita Mji tisini na nane (98)na kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita
tumepata mia mbili thelasini na Nne(234)”Alisema Luhumbi.
Hata hivyo Mhandisi Luhumbi ameiagiza TAKUKURU pamoja na
vyombo vya dola kuwakamata wote waliohusika na usambazaji wa dawa hizo vikiwemo
na vikosi kazi ngazi ya kijiji kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Takukuru mkoani Geita Bw Thobias Ndaro alisema
wanaendesha msako kuwabaini wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo kwenye
maduka.
Post A Comment: