![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Akizungumza na waandishi juu ya msako ambao wamefanya na kukamata vwaharifu 15. |
Vitu ambavyo avijatambuliwa. |
![]() |
Moja kati ya watu ambao wanasadikika kuiba kwenye duka la Nguo akiwa amepigwa na wananchi.
Na,Joel Maduka,Geita.
|
Vitendo vya uhalifu Mkoani Geita
, vikiwemo vya uporaji wa simu na vitu vya ndani kama Televisheni na Redio vimezidi kukithiri ambapo Jeshi la Polisi hadi
sasa linawashikiliwa watu 15 kutokana na vitendo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema kutokana
na msako walioufanya tarehe 28 February
Mwaka huu hadi March 6 mwaka wamewakamata watuhumiwa na vitu mbalimbali.
Kamanda Mponjoli alisema vitu ambavyo
hadi sasa havitajatambuliwa ni
televisheni Sita(6) , Redio mbili(2) za Sub woofer, Spika mbili (2)na
simu Nne(4) pamoja na Deki moja (1).
“Vitu ambavyo havijatambuliwa hadi sasa
ni Televisheni flat screen LG nchi 42, televisheni flat screen home base nchi
24, Televisheni flat screen aborder nchi 49, televisheni flat screen aborder
nchi19, televisheni flat screen tandar 19, televisheni flat screen Mobisol nchi
19,Sub woofer aborder 1,Sub woofer Seaoeano 1, Simu ya Tecno W4, Tecno C8, Tecno
Boom J8, Blackberry Q10, Laptop HP 1,DVD Deck 1”alisema Kamanda Mponjoli.
Kamanda Mponjoli ametaja tukio jingine
ni la Bw Charles Masangwa ambaye aliuawa
kwa kupigwa na fimbo kifuani na Mashaka Sinzya (65)hali iliyosababisha akimbizwe katika kituo
cha afya Katoro baada ya maumivu makali kabla ya kufariki
Baadhi ya wananchi Mkoani humo
wameendelea kusikitishwa na vitendo vya wizi kukithiri hali inayosababisha hali
tete ya kiusalama kwenye makazi ya watu
Hata hivyo Kamanda Mponjoli ametoa wito
kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kwa ajili ya kutambua vitu vyao.
Post A Comment: