Nyumba za askari polisi wilayani Arusha. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba akibadirishana mawazo na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu
Nchemba ametembelea kukagua ujenzi wa
nyumba za polisi wilaya ya Arusha ambazo ziliungua kwa ajali ya moto uliyotokea
mwaka jana umefikiaje mpaka sasa na kuridhika na hatua iliyofikia.
Dkt mwigulu amesema aridhika na hatua
iliyofikia ya ujenzi wa nyumba za askari polisi ambazo ni za kisasa kabisa na
kupongeza hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huu
uanze mala moja, pia mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na wafanyabiashara wa
Arusha kusaidia ujenzi wa nyumba hizo mpaka sasa ulipo kamilika kwani
walichukua hatua mapema tupale moto ulipotokea.
"Leo hii mmeona nyumba hizi za kisasa
ambazo zitafanya askari wangu kuanza kupigia selfie katika nyumba zao kwamba
hapa ndipo ninapokaa, ili ni jambo kama waziri na mshukuru sana Rais na
litaongeza morali ya kuendelea kufanya kazi nzuri wanayoifanya" Waziri
Mwigulup
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
amemshukuru waziri Mwigulu kwa msaada wake wa kufanikisha ujenzi huo
unafanukiwa na kufikia hapo kwani kama waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani
amekua karibu nao sana na kukagua kila hatua inayofikiwa.
RC Gambo ameongeza kusema kuwa kwasasa
wamemuomba waziri Mwigulu awasaidie gari la polisi katika kituo cha polisi
murieti na amekubali kuwasaidia kuwaletea gari ili kusaidia kupunguza matukio
ya kiharifu maeneo hayo kwani kwasasa mji huo watu wengi wanaishi maeneo hayo
na askari wanategemea gari linalotoka kituo kikuu cha polisi Arusha.
Post A Comment: