GGM YATOA MSAADA KWA MATIBABU KWA WAGONJWA WA MIDOMO SUNGURA

Share it:
Mgodi wa Dhahabu wa Geita GGM kwa mara nyingine limefanya zoezi la kuwasaidia wakazi wa Geita wenye matatizo ya mdomo sungura na wenye uvimbe kwenda kufanyiwa upasuaji jijini mwanza katika Hospitali ya Sekoture ikiwa ni muendelezo wa kusaidia jamii inayowazunguka katika kuwapa huduma mbalimbali za kiafya wananchi .
Zoezi la kuwasaidia  wenye midomo sungura ufanyika kwa mwaka mara mbili ambapo kwa mwezi huu wa nne jumla ya watu wazima pamoja na watoto ni 25 wamepata nafasi ya kwenda kutibiwa.
Akiwaaga baadhi ya wagonjwa ambao wanatarajia kwenda kufanyiwa upasuaji kwenye Hospitali ya Sekoture Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewataka watu wengine kuwa na upendo na umoja ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mtu ambaye anatatizo hilo pindi anapoitajika.
Ni zaidi ya watu laki saba wamekwisha kutibiwa tangu zoezi lianze mwaka 2014 .
Share it:

JOEL MADUKA

Post A Comment:

Also Read

MIAKA 22 BILA MV BUKOBA

MV Bukoba ilikuwa moja ya meli kubwa katika ziwa Victoria. Ilikuwa ina uwezo wa kusafirisha watu zaidi ya 400 na tani

JOEL MADUKA