Mkuu wa mkoa wa Mwanza(Kulia)John Mongela akifurahia na Afisa biashara wa NMB Bw,Abdulmajid Nsekela baada ya kuzindua tawi la Igoma.
Katika kuhakikisha kuwa inatambua mchango wa wananchi ambao
wamekuwa wakitumia huduma za Kibenki,NMB Benki wamekuwaja na huduma ya mikopo
ambayo inawahusu wananchi wa kipato cha chini ambayo itawasaidia kuinua uchumi
wa biashara ndogo ambazo wamekuwa wakizifanya.
Akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye
shughuli ya ufunguaji wa tawi jipya la Igoma Jijini Mwanza ,Afisa Mkuu wa
Biashara wa NMB,Bw Abdulmajid Nsekela,amesema kuwa wameendelea kutumia kauli mbiu ya karibu yako
kwa maana kuwa karibu na mteja kwa kutoa huduma za kibenki ,kumshauri mteja
kupata huduma hizo na kutengeneza bidhaa nzuri ili kupata mlaji kulingana na
mahitaji tofauti tofauti ya wateja.
Aidha ameongezea kuwa hadi sasa Benki hiyo inamawakala 5000
na kwa mkoa wa mwanza Pekee inamawakala takribani 200 na kwa igoma wapo saba
ingawa kumekuwepo na orodha ndefu ya baadhi ya wafanyabiashara kuomba kuwa
mawakala.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela amesema kuwa
serikali inatambua na kutoa kipaumbele katika kuendeleza sekta ya Benki nchini.
Na kwamba anatambua kuwa kazi hiyo ya kuwahudumia wananchi
ni jambo nzuri na la busara ikiwa ni pamoja na kuendelea kujitolea vifaa mbali
mbali kwenye ngazi ya afya na sekta ya
elimu.
|
Post A Comment: