Mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Woman Promotion Center ,Bi, Walta Caros akizungumza na waandishi wa habari juu ya sheria ya vitendo vya kikatili kwa mwanamke.
Hofu na kutojiamini ni miongoni mwa sababu za wanawake wengi
wanaofanyiwa ukatili kushindwa kutoa taarifa na kujikuta wakipoteza haki zao
ikiwemo kudhurumia baadhi ya mirathi pindi waume zao wanapofariki.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha Shirika lisilo la
kiserikali la Woman Promotion Centre na maafisa ustawi wa jamii, watendaji wa
mitaa na kata pamoja na Madiwani wa halmashauri za mkoa wa Geita ili kujadili
mapungufu ya sera na sheria za nchi zinazohusu masuala ya kijinsia na haki za
wanawake.
Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya mji wa Geita Bi
Mariam John amesema wanawake wengi wanahofia pale wanapoambiwa kesi zipelekwe
mahakamani hali inayosababisha wengi wao kuendelea kunyanyasika .
“Tatizo kubwa ambalo limeendelea kuwakuta wanawake wengi ni
kuendelea kuwa wasili kwa maana ya kutokutoa taarifa ambazo zitasaidia
kufikishwa kwenye ngazi za kisheria na hata tunapotaka kufikisha kwenye ngazi
hizo wengine wamekuwa wakiogopa”Alisema Mariam.
Mwanasheria wa Shirika hilo Bi Walta Carlos amesema kuna
umuhimu wa kuwepo kwa sheria au sera itakayozungumzia ukatili kwa wanawake kwa
kuwa kumeendelea kuwepo kesi nyingi za ukatili.
“Nadhini ni wakati umefika kwa serikali kuona umuhimu wa
kuwepo kwa sera au sheria ambayo itasimamia na kuzungumzia kwa marefu na mapana
suala la wanawake na wasichana ambao wameendelea kufanyiwa ukatili hii ni
kutokana na sheria iliyopo kwa sasa kuwa na mapungufu mengi”Alisema Mwanasheria
Walta.
|
Post A Comment: