![]() |
Binti ambaye amekutwa akiwa nyumbani kwa Mwalimu wake ambaye jina lake tunalihifadhi. |
![]() |
Bw Francis Andrea ni mzazi wa Mwanafunzi akielezea kusikitishwa kwake na kitendo cha Mwalimu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Binti yake. |
Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Bugando Kata ya Nzera
Wilayani Geita anashikiliwa na Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma za kufanya
mapenzi na mwanafunzi wake wa kidato cha Pili.
Imeelezwa kuwa Mwl huyo Noel Seleman amekuwa na mahusiano ya
kimapenzi na Mwanafunzi wake kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
Bw Francis Andrea ni mzazi wa Mwanafunzi huyo ameeleza
kusikitishwa na kitendo cha Mwl huyo huku akiiomba serikali imsaidie.
“Ni muda nilikuwa nikisikia kuwa anamahusiano na mwalimu
lakini siku hiyo aliondoka asubuhi niliporudi Nyumbani nikamuuliza mama yake
akaniambia alimtuma lakini jambo la kusngaza tangu saa nne hadi saa nane
alikuwa ajafika nyumbani ndio nikachukua maamuzi ya kumwambia mdogo wake ambaye
alikuwa naye kuwa dada yako yupo wapi alinipeleka na kunionesha mimi ilibidi
nirudi na kuwachukua vijana sita na wanawake wane tukaenda kumkamata baada ya
kumkamata tulimwita balozi wa eneo hilo akashuhudia uovu wa Mwalimu”Alisema Bw
Francis.
Mama wa Mwanafunzi huyo Bi Joyce Katambi amesema mara kwa mara amekuwa akimkanya binti
yake kujihusisha na mapenzi akiwa bado anasoma lakini amekuwa amsikilizi hali
ambayo imepelekea kujikuta akikamatwa na mwalimu wake.
Agdes Charles amesema amekuwa akimuona Binti huyo akija na
kuondoka kwa mwalimu huyo na hata wanapomuzuhia amekuwa akiwatukana na
kuwaambia waache kumfuatilia.
Balozi wa eneo hilo Bw Shaaban Majaliwa amesema walipozungumza na mwanafunzi huyo alikiri kuwa
na mhusiano na Mwl wake tangu akiwa kidato cha kwanza.
Kwa upande wake Mwanafunzi huyo mwenye miaka 17 alipohojiwa
na mtandao huu amekanusha kuwa na
mahusiano na Mwl wake na kwamba alikwenda nyumbani kwake kumjulia hali baada ya
kupata taarifa kuwa amepatwa na ajali.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Bw Mponjoli Mwabulambo
amesema tukio hilo limelitokea tarehe 13 mwezi huu majira ya saa nane mchana na
mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Hata hivyo Mzazi wa mwanafunzi huyo amedai kuwa kuna dalili
za tukio hilo kutaka kupotoshwa ukweli wake ili haki isipatikane
Post A Comment: