MWAMUZI ASHUTUMIWA KUHODHI MCHEZO WA POLISI NA STENDI MKOANI GEITA.

Share it:
Mechi ya Polisi na Stendi zote za Mkoani Geita Katika mchezo wa wiki ya nenda kwa usalama.
Wachezaji wa Timu zote mbili na waamuzi wa mchezo huo wakiingia uwanjani.

Mgeni Rasimi ambae ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo akikagua vikosi hivyo.


Baada ya ukaguzi akapata wasaa wa kuzungumza na vikosi hivyo huku akiwasihii kuwa na nidhamu katika michezo yote.

Kikosi cha Polisi Kikimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi.

Kikosi cha Stendi nacho kikiwa makini kufatilia maagizo ya mgeni rasmi

Mchezo ni upendo na nifuraha  Timu zote mbili zikisalimiana.


Wachezaji wakiendelea na mchezo kwa kasi kubwa zaidi.

Chenga za akili na zenyewe zilikuwemo katika mechi hiyo.

Mashambulizi yakiendelea.




Michuano ya ligi ya nenda kwa usalama imezinduliwa siku ya jana katika  viwanja vya shule ya sekondari  kalangalala na kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo.

Uzinduzi wa mashindano hayo ya mpira wa miguu yamezikutanisha timu mbili katika ufumbuzi ambazo ni Polisi na Stendi zote za mkoani Geita,Michuano hiyo ilianza saa 11:20 jioni kwa kuzikutanisha timu hizo ambapo katika kipindi cha kwanza timu ya polisi ilionesha kuwa na kasi kubwa katika mchezo huo hali ambayo ilipelekea mchezaji wa timu ya polisi Shaban Kazolwa kuipatia bao la kwanza timu hiyo katika dk10 kipindi cha kwanza tangu kuanza.

Kutokana na  kasi ambayo walikwenda nayo Timu ya Polisi, Stendi haikukubali kushindwa ambapo nayenyewe iliweza kuonesha nguvu zaidi dhidi ya timu ya Polisi na katika Dk 33 waliweza kusawazisha goli ambalo lilifungwa na Dumzi Lukemo.


Hadi Dk,90 zinakamilika za mchezo timu zote mbili zilikuwa sare  kwa  goli moja kila timu hali ambayo ilipelekea waweze kwenda matuta lakini hata hivyo hali ya sintofahamu iliweza kujitokeza kutokana na kutokuwa na maelewano ambapo timu ya stendi ili mlalamikia kocha kuhodhi  mechi hiyo kutokana na kwamba hata wakati wa kwenda matuta alionekana kuwapendelea timu ya Polisi.hali hiyo ilipelekea timu ya stendi kugoma kupiga penati na kuomba mechi hiyo irudiwe lakini mwamuzi wa mchezo huo aliweza kuwatangaza polisi kuwa ndiyo washindi wa mechi hiyo.

Imeandaliwa na Joel Maduka


Share it:

michezo

Post A Comment: