|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizungumza na watendaji katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Geita. |
|
Mkurugenzi wa Halamshauri ya wilaya Geita Ali Kidwaka, |
|
Kidwaka akiwaagiza watendaji kuwa waadirifu na kujituma kuwatumikiwa wananchi. |
|
Mganga wa Wilaya ya Geita ,Raphael Mhana akielezea umuhimu wa kutunza mazingira kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. |
|
Felix Jackson mhasibu wa halmashauri ya wilaya ya Geita . |
|
Afisa utumishi wa wilaya ya Geita,Beatrice Agustino akiwaagiza watumishi kuvaa mavazi ya heshima pindi wanapokuwa kazini. |
GEITA:Mkuu
wa Wilaya ya Geita,Hermani Kapufi,amewaagiza maafisa watendaji wa kata,vijiji na vitongoji kushughulika na
wale wote ambao watabainika wamewapatia ujauzito wanafunzi ambao bado wapo
masomoni.
Kauli hiyo
,ameisema wakati alipokutana na watendaji katika kikao cha pamoja kilichofanyika
katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Geita ambacho kilikuwa kimelenga kutatua
changamoto za watendaji wa kata,vijiji na vitongoji.
Amesema kuwa
suala la baadhi ya watu kuendelea kuwapa mimba watoto wa shule limekuwa ni changamoto ambayo imesababisha
kukatisha ndoto za baadhi ya wanafunzi kwa kuwashawishi kwa vitu vidogo na
mwisho wa siku kuwapotezea ndoto zao pamoja na mlengo waliyojiwekea.
“Natambua
kuwa kuna tatizo kubwa linaloendelea kwa maeneo ya hapa wilayani kwa watu
kuendelea kuwapa mimba wanafunzi na mwisho wa siku hakuna sheria yoyote
inayochukuliwa mimi nikiwa kama Mkuu wa wilaya hii ninawaagiza watendaji wote
kuwashughulikia wale wote ambao wanatabia ya namna hiyo serikali inawekeza
fedha nyingi sana kwa wanafunzi leo hii wanatokea baadhi ya watu kukatisha
ndoto zao kamwe hatuwezi kuwafumbia macho watu wenye tabia za namna hiyo”alisema
Kapufi.
Aidha kwa
upande wao watendaji wamesema kuwa
matatizo ya baadhi ya watu kuwapa mimba wanafunzi yapo mengi sana katika maeneo
wanayo yaongoza na kutokana na agizo hilo wanaamini kuwa wataweza kuwaadhibu
wale ambao wamekuwa na tabia za namna hiyo.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
Post A Comment: