Wanafunzi wa madarasa ya
awali la kwanza na walioko nje ya mfumo wa elimu MEMKWA katika
halmashauri ya mji wa Geita Mkoani humo wameendelea kunufaika na mpango wa KKK
tatu ikiwa ni mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Kusoma, Kuandika
na kuhesabu.
Hatua hiyo inatokana na serikali kutambua kuwa elimu ni
msingi kwa kila mtoto ambaye kwa namna moja au nyingine alikosa nafasi ya
kujiunga wakati akiwa katika umri ambao unatakiwa hivyo kupitia Darasa la MEMKWA litamwezesha kufikia malengo
yake.
Kwa kuzingatia kuwa elimu ni silaha muhimu kumkomboa mtoto kifikra, serikali ilianzisha programu
ya Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa Watoto
Walioikosa (MEMKWA) ili kuwawezesha watoto kupata elimu nje ya mfumo rasmi.
Marko John ni moja kati ya wanafunzi wa shule ya msingi
mseto amesema sababu ya yeye kuchelewa shule ni kutokana na wazazi wake
kutafarukiana na kujikuta akiishi kwa bibi yake kijijini ambaye na yeye akuwa
na uwezo wa kumtunza.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi,Grace Mutabuzi ameelezea changamoto ambazo zimekuwa
zikiwakumba watoto wanaosoma madarasa ya MEMKWA ni pamojana na wengi wao kuwa
na majukumu ya kifamilia kwa maana ya uangalizi wa familia zao.
Afisa Elimu msingi Halmashauri ya Mji wa Geita Yese Kanyuma
amesema kumekuwepo na mafanikio makubwa kwa baadhi ya wanafunzi wa darasa la
MEMKWA ni kutokana na ushirikiano baina ya jamii ambayo inatamani kumuona mtoto
anaelimika.
Programu ya MEMKWA ilianzishwa kwa majaribio kati ya mwaka
1999 hadi 2002 katika wilaya za Musoma Vijijini, Kisarawe, Ngara, Masasi na
Songea Vijijini. Programu hiyo
ilipoonyesha mafanikio, mwaka 2003 serikali ilianzisha madarasa ya MEMKWA
katika shule za msingi nchi nzima.
|
Post A Comment: