Felix Joseph akielezea kuchukizwa na namna ambavyo walinzi na wauguzi katika hosptali hiyo wamekuwa na majibu mabaya kwa watu wanaokuja kuwasalimia ndugu zao na wagonjwa pia hali ambayo imekuwa ikiwanyima amani wagonjwa na wale ambao wanakuwa wakiwauguza hosptalini hapo.
Familia yagoma
kuchukua mwili wa marehemu wa
mzazi wao (maiti) kwa kile kinachodaiwa
wauguzi wa hospitali teule ya rufaa ya mkoa
wa Geita kuwa na majibu machafu kwa wagonjwa.
Akizungumza
na mtandao wa madukaonline katika mazingira ya hospitali hiyo mmoja kati
ya wanafamilia ambae amefiwa na baba
yake mzazi,Bahati Chihula mkazi wa
kijiji cha Kishinda kata ya Kamhanga wilayani Geita.
Amesema kuwa walimpeleka Baba yao siku ya jumatano ya
tarehe 5 mwezi huu kwa lengo la kupatiwa matibabu ya tenzi dume lakini jambo la
kusikitisha alikutana na huduma
zisizostahili za wauguzi hali
ambayo imepelekea mzazi wake kupoteza maisha kutokana na kukosa
huduma nzuri za afya.
“Tulifukuzwa
katika hodi ya wagonjwa kwa madai kuwa hatutakiwi kukaa katoioka hodi hiyo na
tulipotoka nje baada ya dakika chache niliporudi nilim kuta mgonjwa wangu yupo
chooni na nilipouliza kwanini mgo njwa wangu yupo choo ni akiwa nagaragara
mhuguzi alionijibu wewe utakiwi kujua nenda zako na kutokana na huduma mbovu za
hospitari hii imepelekea kuondoa uhai wa baba yangu kwani hakuwa maututi sana
na sisi kama family hatutachukua maiti paka sheria ifate mkondo wake”Alisema
Bahati.
Hata hivyo
moja kati ya wananchi ambae ana mgonjwa
anaye muuguza katika hospitali hiyo Felix
Joseph ameeleza tatizo kubwa ni
walinzi pamoja na wauguzi kwani wamekuwa
wakiwatusi wagonjwa na wananchi wanaokuwa
wakifika katika hosptali hiyo.
Kutokana na
uzito wa swala hilo mbunge wa Geita vijijini
Joseph Msukuma amefikisha malalamiko hayo katika kikao cha sita cha
kamati ya ushauri ya mkoa kutaka
kujua utawala bora ukoje katika hospitali hiyo na
juu ya hatua zilizochukuliwa na
mganga mkuu wa mkoa dhidi ya mgonjwa aliyefia chooni .
“Mwenyekiti
nilikuwa nataka kuuliza kuhusiana na utawala bora kwenye hopstari ya Mkoa Jana
mpiga kula wangu alimleta baba yake mzazi hospitarini hapo cha kusikitisha ni
kwamba alifukuzwa na kutolewa nje je ni haki naomba mganga mkuu hatujibu
ameshachukua maamuzi gani juu ya wale ambao wameshiriki katika kitendo hicho
cha unyanyasaji”aliuliza Msukuma.
Akijibu
kuhusiana na tuhuma hizo za kumwacha mgonjwa
na mwisho wa siku akapoteza uhai wake mganga mkuu wa mkoa Joseph Kasala,amefafanua kuwa walipewa mgonjwa huyo
akiwa anasumbuliwa na tenzi dume na
kwamba wakati daktari ambae alitakiwa kumfanyia upasuaji alishindwa kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.
Sanjari na hayo mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali
Mstafu Ezekiel Kyunga amemwagiza mganga mkuu kwenda
hospitalini hapo na kupata habari za kina na kujua ni
nani ambae amefanya uzembe wa namna hiyo na
kama mtu akibainika hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake.
|
Post A Comment: