Wavuvi wa mwalo wa Makatani kata ya Nkome wilayani Geita wakiendelea na maandalizi kwaajili ya kwenda kwenye shughuli ya uvuaji wa dagaa. |
Dhana za uvuvi ambazo wamelalamikiwa kuwa zinakamatwa na maafisa uvuvi kwa madai kuwa zinashiri kwenye suala la uvuvi haramu. |
Mzee Yohana Kulwa akielezea masikitiko yake kutokana na suala kuendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya uvuvi bila ya kuwa na makosa yoyote. |
Wavuvi wa Mwalo wa makatani Kata ya nkome Wilaya na Mkoa wa
Geita,wamelalamikia kuonewa na watu kutoka idara ya uvuvi kutokana na kuendelea
kuwakamata na kuwapiga faini pasipokuwa na makosa yoyote yale hali ambayo
imeendelea kuwatia hofu pindi wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.
Hatua hiyo imekuja ni kutokana na msako ambao unaendelea
ziwa Viktoria wa kuwakamata watu ambao wameendelea kujihusisha na shughuli za
uvuvi haramu.
Wakizungumza na mtandao huu ,baadhi ya wavuvi hao wamesema kuwa pamoja na kuendelea kutii
sheria kwa kutumia zana za uvuvi ambazo zinakubalika kwa mujibu wa sheria bado
wameendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya uvuvi.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho ,Bi Anna Peter na Mwenyekiti wa BMU Bw,Peter John
wamedai kutokushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya kukamata watu hao na
kwamba elimu bado ni tatizo kwa wavuvi wengi kutokujua ni zana
zipi ambazo zinatumika kwenye shughuli zao kutokana na kutokupewa elimu.
Hata hivyo kwa upande wake diwani wa kata hiyo,Masumbuko
Nsembe amesema malalamiko ya wavuvi hao amekwisha kuyapeleka halmashauri na
kwamba hadi sasa yanafanyiwa kazi.
Mtandao huu umemtafuta Mkuu wa oparesheni hiyo,Bw Roman Mkenda kwa njia ya simu
ambapo amesema kuwa baadhi ya wavuvi
wamekuwa wakikimbia pindi wanapowaona hali ambayo inasababisha wao kujua kuwa ni mvuvi haramu na kwamba suala la elimu
wamekuwa wakilitoa pindi mtu anapoomba kibali cha kutaka kuwa mvuvi.
Post A Comment: