Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akikemea vikali tabia ya baadhi ya wazazi kuendelea kuwatumikisha watoto kuwa watafutaji badala ya wao kutafuta.
Kumekuwepo na wimbi kubwa la watoto kuingia kwenye maeneo ya
mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM),kwa madai baadhi yao wamekuwa wakitumwa na
wazazi wao na walezi kwa ajili ya kuokota vyuma chakavu na mawe ya
dhahabu maarufu kwa jina la magwangala hali ambayo inaweza
kusababisha kutokea kwa hatari kwa watoto hao kutokana na maeneo
mengi kutokuwa salama.
Hali hiyo inatokana na wazazi na walezi kushindwa kufuatilia
kwa umakini muda wa wengi kushindwa kujali masomo na kujikuta
wakitumia njia za panya kuingia kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya geita kata ya
mtakuja mjini humo.
Wakizungumza na
mtandao huu kwenye eneo la kutupia
uchafu ndani ya mgodi huo baadhi ya watoto hao wamesema kuwa wamekuwa wakiingia
kwa ajili ya kuwinda wanyama pori ambao wanapatikana kwenye maeneo ya mgodi
huo.
“Sisi tunaingia humu kwa nia tu ya kuwinda wanyama pori wala
sio masuala ya kuogota vyuma na mangwangala”Alisema mmoja wa watoto hao.
Afisa mahusiano wa mgodi huo bw,Mussa Shunashu amewashauri watoto
hao ambao wamekuwa wakiingia kwenye maeneo hayo kuachana na tabia hiyo na
badala yake watumie muda huo kujisomea kwani kufanya hivyo wanaweza kujikuta
wanaingia kwenye matatizo kutokana na maeneo mengi ya mgodi kuwa hatari kwa
maisha ya watoto hao.
Baadhi ya wazazi ambao wamezungumza na mtandao huu
umesikitishwa na kitendo cha watoto kwani wengi wao wamekuwa wakitoroka
nyumbani pasipo wazazi kujua wanakwenda wapi.
Mwenyekiti wa mtaa wa kompaundi ambao unauzunguka
mgodi huo,bw ediga Onyango,amewataka walimu wakuu wa shule za msingi kutoa
taarifa kwenye uongozi wa mtaa pamoja na wazazi kuachana tabia ya kuwaagiza
watoto kwenye maeneo ya mgodini.
Aidha mkuu wa wilaya
ya Geita Mwl,Herman Kapufi amewaonya wazazi wenye tabia hizo na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa mzazi ambaye
hatagundulika anamuagiza mtoto wake kwenye maeneo ya mgodi wa GGM.
Takwimu za watoto ambao wamekuwa wakiingia mgodini wa ggm
zimeendelea kupanda ambapo kwa wastani kila mwezi watoto sitini(60)
wenye umri wa miaka sita na saba hadi 10 wameendelea kuingia kwenye maeneo hayo
hatarishi.
|
Post A Comment: