Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza juu ya mikakati ya kuwasaidia wananchi na tatizo la kukosekana kwa Daraja .
Wananchi wa Kijiji cha Nyakagwe
kata ya Butobera Wilayani Geita wameiomba serikali kuwatengenezea daraja la
kuvukia kwenye mto unaopita kijijini
hapo kutokana na sasa hivi kujikuta wakipata shida pindi maji yanapojaa kwenye
eneo hilo.
Baadhi ya wanakijiji ambao
wamezungumza na mtandao huu wameelezea kuwa wamekuwa wakipata shida kubwa pindi
mvua zinaponyesha na kusababisha wanafunzi kushindwa kwenda masomoni pindi mto huo unapojaa maji.
“Pindi mvua zinaponyesha
mwandishi watoto wetu wanashindwa kwenda masomoni kwani hali inakuwa ni mbaya
na maji yana jaa sana kwenye haya maeneo ya juu hivyo tunajikuta tunashindwa
namna ya kufanya tunabaki kuwashauri wanafunzi kutokwenda kwenye masomo lakini
tunaamini kama serikali itasikia kilio chetu ikatusaidia juu ya hili tutakuwa
tumenufaika”Alisema Mzee John Mabisa.
Hata hivyo diwani wa Kata hiyo,Bw
Hemed Swalehe amesema jitihada ambazo amezifanya kwa sasa ni
kuwasiliana na wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Hili waweze
kufika na kujionea tatizo hilo waone namna ambavyo wanaweza kuwasaidia wananchi
hao ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl
Herman Kapufi amefika kwenye eneo hilo na kujionea tatizo na kuahaidi
kuwasiliana na meneja wa TARURA ili aweze kuja na kuona namna ya kutatua tatizo
hilo.
“Niseme tu kwamba nitahakikisha
Meneja wa TARURA wa Mkoa anakuja na kuona namna ambavyo wanaweza kusaidia
ujenzi wa daraja hili ambalo limekuwa ni tatizo la Muda mrefu kwa wananchi wa
vijiji hivi viwili kwa maana Butobela na Nyakagwe”Alisema DC Kapufi.
|
Post A Comment: