KANUNI BORA ZA MAFANIKIO HIZI HAPA

Share it:
I

li uweze kufanikiwa unahitaji kuzifahamu kanuni hizi mbili ambazo zitakusaidia kutoka sehemu moja hadi nyingnine. Na endapo utazipuuza utaendelea kuwa mkwasi maisha yako yote, nasema hivi kwa sababu kanuni hizi ni za uhakika katika safari yako ya mafanikio.

1. Jiamini wewe mwenyewe.
Mafanikio yote makubwa huja kutokana na kujiamini wewe mwenyewe na kuua hofu zote zinazokukwamisha. Unapojiamini unajijengea nafasi nzuri sana ya kufikia mafanikio yako makubwa. Ni muhimu sana kuweka jitihada zako wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa huku ukijiamini. Hata kama unachukua ushauri kwa wengine ni jambo zuri sana lakini kikubwa jiamini.

Ili uweze kuongeza uwezo mkubwa wa kujiamini ni vyema kuwa na mawazo chanya yenye kuleta maono ya kufanikiwa hapo baadae. Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa jiamini kuwa unaweza ama hakika utafanikiwa maisha siyo magumu kihivyo kama wengi tunavyofikiri ila sisi ndio wagumu na daima siku zote kitu rahisi ndicho sahihi.

2. Acha kusikiliza maneno ya watu wanaokukatisha tamaa.
Wapo baadhi ya watu ambao wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu wengine tamaa. Hivyo basi kama wewe ni kweli unahitaji mafanikio najua yapo mengi yatasemwa juu yako kwa ajili ya kukuvunja moyo. Wewe wasikilize tu watu hao lakini achana na mawazo hasi ambayo hayana tija kimafanikio na sumu kubwa kwako.

Siku zote jifunze kuwa ni mtu wa kusikiliza mawazo chanya yenye kuleta njia sahihi ya kuona maono ya kimafaniko. Kuwa makini katika kuchagua marafiki sahihi wenye mawazo yakinifu yenye kuleta mtazamo wa kimafaniko. Achana na watu wataokurudisha nyuma kimafanikio kwa namna yoyote ile.
Share it:

Darasa huru

Post A Comment: