Bajaj zikiwa zimepakiwa na waendeshaji mjini Geita baada ya kuwa na madai ya kuonewa na askari. |
Bw,Joseph Dotto ambaye ni mwendesha bajaji mjini Geita akilalamika juu ya kamata kamata ambayo inaendelea mjini humo. |
Waendesha Bajaji Mjini Geita Mkoani Humo wamelilalamikia
jeshi la Polisi kuendelea kuwakamata pasipokujua makosa yao ni nini na kujikuta
wakishindwa kuendelea kufanya kazi zao kwa amani hali ambayo imepelekea
kutokuendelea na kazi zao za usafirishaji wa abiria.
Wamesema hali hiyo imeendelea kuwaathiri kutokana na wengi
wao kukopa bajaji hizo na kutegemea kufanya kazi hili waweze kurudisha madeni
ambayo wanadaiwa na kampuni za usafiri huo.
Bajaj ndio usafiri
maarufu mjini Geita kwa mizunguko ya hapa na pale lakini
Waendesha Bajaji wamejikuta wakisitisha kuendelea kufanya kazi zao kutokana na
kuwa na malalamiko ya kukamatwa na
kutozwa faini kubwa bila ya kujua makosa yao.
“tumeendelea kukamatwa na
kupigwa faini pasipokujua makosa yetu ni nini hata tukiuliza hatujibiwi
tunakamatwa na kuambiwa twende kituoni tena na askari ambao wanakuwa wamevaa
nguo za kirahia je hiyo ni haki kweli sasa hivi ninasiku mbili sifanyi kazi
watoto wangu wamelala na njaa sijajua tatizo ni nini hadi kufikia hatua ya
kukamata bajaji zetu”Alisema Bw,Mussa Kisoke.
Hata hivyo baadhi yao
wameelezea kuwa pamoja na kukamilisha usajili wa bajaji zao na kuwa na kila
kitu bado wameendelea kukutana na dhoruba la kamata kamata inayoendelea kwa
sasa mjini humo.
“Sisi hizi bajaji
tumezikopa na tunarejesha marejesho kwa wiki na isitoshe zingine zimekamilisha
kila kitu kwa maana ya bima,Sumatra na leseni lakini tunakamatwa na kupigwa
faini kiuweli tunaumia sana”Alisema Joseph Dotto.
Kutokana na malalamiko
hayo kuliangukia Jeshi la Polisi kamanda
wa Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo amesema msoko unaendelea kutokana na
mambo ya ukiukaji masuala ya usalama barabarani na kwamba wataendelea
kuwakamata wale wote ambao wameendelea kukiuka kanuni na taratibu za usalama
Barabarani.
“Sababu ni uwegeshaji
hivyo barabarani kwa maana wanasimama sehemu ambazo sio sahihi ninachotaka
kusema kwamba hatuwaonei na tumeshakaa tukaongea nao maana tumeshatoa elimu na
utaki kutuelewa tutachukua hatua”Alisema Kamanda Mponjoli.
Post A Comment: