Katibu wa Mbunge wa Geita Mjini ,Mariam Mkaka akiwasisitiza wanafunzi hususani ni wa kike kusoma kwa Bidii zaidi kutokana na kwamba serikali imetatua changamoto yao kwa kujenga Mabweni.
Picha zote na Joel Maduka wa Maduka Online.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita Meja Jenereli Mstaafu Ezekiel
Kyunga amezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitano ambapo mitatu ni
vituo vya afya na viwili ni shule moja na Mabweni kwenye shule ya sekondari
Kasamwa.
Akielezea
Miradi hiyo yote Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mhandisi Modest Aporinali amesema bajeti ambayo waliyonayo kwa kila
kituo cha afya wametenga kiasi cha sh ,Milioni Miamoja na kwamba mahitaji ni
vituo vya afya kumi na kwasasa ni vituo viwili ambavyo vinafanya kazi.
“Ni kweli
Halamshauri yetu inauwitaji Mkubwa sana wa Vituo vya afya ingawa kwa sasa
tunavyo vituo viwili ambavyo ni Nyankumbu na Kasamwa ambavyo vinafanya kazi
hata hivyo mmeona tumezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye vituo vitatu
ambapo ni Mpomvu,Nyanguku na Shiloleli tutaendelea na jitihada kwa kutumia
mapato yetu ya ndani ili kupunguza changamoto ya vituo vya afya hata hivyo GGM
wametupa msaada kama milioni mia moja kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya
Mgusu”Alisema Modest.
Hata Hivyo
Mkurugenzi Modest ametaja miradi ya shule ambazo zimewekewa mawe ya msingi kuwa
ni shule ya Msingi Tumaini pamoja na Mabweni kwenye shule ya sekondari Kasamwa
na kwamba wanaendelea na juhudi ya kupambana na changamoto za elimu kwenye
Halmashauri ya Mji.
Mkuu wa Mkoa
,Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga ,amesisitiza kuwa serikali inafanya
juhudi za kuwashirikisha wananchi katika swala la maendeleo na kwamba
wanatakiwa kuwa na mwitikio katika swala la maendeleo kwa wao kama wananchi kwa kujitolea bila ya kusubilia serikali huku
akiwataka baadhi ya watu kutokuwa na desturi ya kulalamika bila ya kufanya
shughuli kwa kushirikiana na Serikali.
Aidha kwa
upande wao wananchi ambao wamezungumza na maduka online Habari wameipongeza
serikali kwa hatua nzuri ya kuwapelekea vituo vya afya kwenye maeneo yao huku
wakielezea changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili kabla ya kuwepo kwa vituo
vya afya kuwa ni umbali mrefu wa kufuata huduma ya afya.
Jumla ya
miradi yote ambayo imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi imeghalimu kiasi cha
Sh,Milioni Mia saba na thelasini na sita pesa ambazo zinatokana na mapato ya
ndani.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE |
Post A Comment: