BENKI YA NMB YAFANIKISHA SIKU YA WAUGUZI MKOANI GEITA

Share it:
Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa  wa NMB Bi Suma Mwainunu Akitoa shukrani kwa wao  kama Benki kushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya siku ya wauguzi Duniani huku akihaidi kwa Kwa Benki yao kuendelea kushirikiana na serikali.
Maandamano ya Wauguzi kutoka Katika Mkoa wa Geita yakiingia kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mbongwe ambapo ndipo yamefanyika maadhimisho kwa ngazi ya Mkoa wa Geita.
Maandamano yakiwa yamesindikizwa na Askari wa usalama  Barabarani pamoja na vijana wa Skauti Wilayani Mbongwe Mkoani Geita.
Vijana wa Skauti wakionesha ukakamavu wakati walipokuwa wakimpokea Mgeni Rasmi katika shughuli ya siku ya wauguzi Duniani.
Burudani ya Ngoma na michezo mbali mbali vikiendelea kwenye viwanja vya shule ya msingi Mbongwe.



Vijana wa Skauti wakiingia uwanjani kwaajili ya kuonesha shughuli za ukakamavu ambazo wamekuwa wakijifunza .
Baadhi ya wadau mbali mbali wakiwemo wauguzi wakiangalia Gwalide kutoka kwa Skauti.



Wauguzi wakisoma kiapo cha uadilifu wakati wa shughuli za maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza na wauguzi pamoja na wananchi juu ya umuhimu wa siku hiyo.

Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa  wa NMB Bi Suma Mwainunu Akitoa neno la Shukrani kwa wananchi  pamoja na wauguzi ambao walikuwa wamekusanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mbongwe.

Wananchi wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi.
Mgeni Rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mwakilishi wa makampuni ambayo yamefadhili shughuli ya siku ya wauguzi kutoka Benki ya NMB,Suma Mwainunu.

Picha na Joel Maduka wa Maduka online.

Benki ya NMB Tawi la Geita limetoa fulana 360 kwenye siku ya Wauguzi Duniani lengo likiwa ni kuendelea na Jitihada zake za kuwa karibu na jamii.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi ambapo Kimkoa yamefanyika Mkoani Geita ,Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa Bi Suma Mwainunu,amesema kuwa Benk hiyo inatambua thamani ya wauguzi na kwamba ndio maana wameamua kushiriki kwa kufadhili fulana hizo.

“Tumejisikia Vizuri sana na hivyo kwa niaba ya NMB tumeweza kushiriki hafla hii kwa kutoa Shilingi Milioni Tatu ambazo zimetumika Kununua Fulana ambazo mnaona wengi Tumezivaaa wauguzi hoyeeeeee”Alisema Bi Mwainunu.

Hata hivyo Bi,Suma Ameongezea kuwa  Benk ya NMB  ipo  karibu na wateja na ndio maana wameshiriki hafla hiyo pamoja na wateja wao.

 Aidha Bi, Suma ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuiamini na kutumia Huduma ambazo zinatolewa na Benk hiyo yenye matawi mbalimbali nchi nzima na pia ametoa wito kwa  uongozi wa Mkoa  kushirikisha Benki ya NMB Katika maswala mbali mbali ya Kijamii nao wakiwa na uwezo wapo tayari kushirikiana nao.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni Rasmi Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ameishukuru Benki ya NMB kwa mchango wake katika kufanikisha sherehe hizo.


IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Share it:

BIASHARA

Post A Comment: