MAGIC FM NA RADIO FIVE ZA FUNGIWA

Share it:
Waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezo ,Nape Nnauye amevifungia kwa muda vituo vya redio five cha arusha pamoja na kituo cha redio cha magic fm cha dar es salaam kwa kile kinachodaiwa vituo hivyo kurusha vipindi vyenye uchocheziAkizungumza  na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam waziri huyo amesema  uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikia baada
kujiridhisha kuwa Redio five katika kipindi cha matukio kilichorushwa tarehe 25 Agosti,2016 muda wa saa 2;00 usiku hadi saa 3;00 usiku ambapo katika kipindi hicho alihojiwa Mbunge wa Arusha Majini,Godbless Lema ambapo alikuwa anatoa maneno ya uchochezi Mbali na Redio five pia ametaja kosa lilipelekea kukifungia kituo cha Magic Fm cha DaresSalaam.Amedai mnamo tarehe 17,Agosti 2016 katika kipindi cha Morning Magic kipindi hicho kilichoruka mda saa 1.00 asubuhi na saa 2.30 katika kipengele cha Kupanga Rangi watangazaji wa kipindi hicho walisikiaka wakitoa maneno anayoeleza kuwa  Rais anavunja
Katiba sasa wananchi wa chini wafanyaje,nao lazima watafanyahivyoKufungiwa kwa vituo hivyo inakuwa ni mwendelezo wa waziri huyo kuvifungia vyombo vya habari ambapo kwa kipindi cha miezi nane ameweza kuyafungia magazeti ya Mawio,mseto yote yanamilikiwa na mbunge wa ubungo ,saed kubenea kwa hoja kuwa  yanaandika habari za uchochezi
Share it:

Post A Comment: