Mgeni rasimi katika mashindano hayo ambae ni diwani wa kata ya Bukoli,Faraji Rajabu akiwapongeza wachezaji timu ya wakongwe. |
Mgeni rasimi akisalimiana na kugagua timu ya Bugogo FC |
Akisalimiana na wachezaji wa timu ya Nchimbi FC |
Mchezo ukiendelea kwa kishindo katika viwanja vya ccm Bukoli. |
Wakifatilia mchezo kwa makini |
Mashabiki wakiwa fatilia kwa makini mpambano. |
Kombe likiwa linasubilia hatakae linyakua |
Mashabiki wakishangilia baada ya ushindi wa nchimbi fc. |
Wachezaji wakisubilia maelekezo ya zawadi. |
Wakati wa zawadi ukawadia sasa. |
Na Joel Maduka Geita.
Michuano Ya Faraji Cup Ambayo Ilikuwa
Inaratibiwa Na Diwani Wa Kata Ya Bukoli,Wilayani Geita,Imemalizika Huku Timu Ambayo Haijawai Kuwa Na Historia Ya
Kuchezea Kichapo Ya Bugogo Fc Imejikuta Ikila Kichapo Cha Mabao Mawili Na Timu Ya Nchimbi Boys Na Yenyewe
Kuambulia Bao Moja Kwenye Dk 40 Kipindi Cha Kwanza.
Michuano Hiyo Ya Ligi Ya Faraji Cup Ilianza
Kwa Mashindano Ya Sarakasi Huku Timu Za Wakongwe Mavetirani Wakikumbushia Mchezo Wa Mpira Wa
Miguu ,Na Saa Kumi Na Dk Hamsini Ndipo Mchezo Ulipoanza Kulindima Katika
Viwanja Vya Ccm,Bukoli.
Mchezo Ulianza Kwa Bashishi Kubwa Sana Kutoka
Kwa Timu Ya Bugogo Ambayo Ilionesha Kushambulia Mchezo Huo Kwa Nguvu Zaidi
Katika Kipindi Cha Kwanza , Dk 40
Marius Joseph
Aliweza Kuipatia Gori La Kwanza Timu Ya Bugogo.
Hadi Wanakwenda Mapumziko Timu Ya Bugogo Fc
Ilionesha Kuwa Juu ,Baada Ya Mapumziko Mchezo Wa Pili Ulianza Kwa Kishindo
Kikubwa Ambacho Kilianzishwa Na Timu Ya Nchimbi Fc Na Ndani Ya Dk 23
Kipindi Cha Pili Peter Dotto,Aliweza
Kuipatia Timu Ya Nchimbi Bao Moja Na Kuwa Sare Ya Bao Moja Kwa Timu Zote
Mbili,Mchezo Uliendelea Na Ndani Ya Dk 36 Katika Kipindi Cha Pili Timu Hiyo
Hiyo Ilipata Bao La Pili Lililofungwa Na Juma Dede Hadi Dk Tisini Zinamalizika
Timu Ya Nchimbi Fc Ilikuwa Ikiongoza Kwa Mabao Mawili Kwa Moja Kutoka Kwa
Bugogo.
Hata Hivyo Mchezo Huo Uligubikwa Na Fujo
Katika Kipindi Cha Pili Ni Baada Ya Mchezaji Wa Timu Ya Bugogo ,Ibrahimu Kadele
Kumpiga Ngumi Ndani Ya Uwanja Robart Steve Hali Ambayo Ilisababisha Mwamuzi Wa
Timu Hizo Mbili Kuwapa Kadi
Nyekundu,Mwingine Aliyepatiwa Kadi Nyekundu Ni Ramadhani Abdu Wa Timu Ya
Nchimbi Fc.
Hata Hivyo Mwandaaji Wa Michezo Hiyo,Ambae Ni
Diwani Wa Kata Ya Bukoli,Faraji Rajab
,Amewataka Wanamichezo Hao Kuungana Hili Kuendeleza Soka La Kata Hiyo.
“Natagemea Kwamba Ndani Ya Miaka Mitano Ya
Uwongozi Wangu Niwapate Vijana
Ambao Watafikia Hatua Ya Kucheza Supa Ligi Ya Vodacom”Alisema
Faraji.
Kocha Wa Timu Ya Nchimbi Boys Fc,Zakaria
Hamad,Alisema Kuwa Siri Kubwa Iliyowafanikisha Kuweza Kupata Ushindi Huo Ni
Mazoezi Ambayo Wamekuwa Wakifanya Mala Kwa Mala.
Katika Michuano Hiyo Mshindi Wa Kwanza
Amepatiwa Kitita Cha Sh,Laki Tatu,Na Kombe Wa Pili Akipatiwa Kiasi Cha Sh Laki
Mbili Na Wa Tatu Laki Moja.
Post A Comment: