Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka miwili mwalimu wa Shule ya Sekondari Msalala, Henry Tagata kwa kosa lakuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh9 milioni.
Akisoma hukumu hiyo mbele ya waendesha mashitaka wa Takukuru, Kelvin Mrusuri akisaidiana na Agustino Mtaki, hakimu Ushindi Swalo alisema kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na waendesha mashitaka wa Takukuru umethibitisha pasipo shaka kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo.
Post A Comment: