Jeshi la
polisi mkoani Geita , limewataka wananchi
katika kuelekea siku kuu ya pasaka pamoja na uzinduzi wa
mwenge Kitaifa, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na
wazazi kuhakikisha usalama na watoto wanapokuwa
kwenye maeneo ya barabara na mitaani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao
makuu ya jeshi la polisi Mkoani humo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli
Mwabulambo alisema katika kipindi hiki cha siku kuu ya pasaka wameimarisha
ulinzi na kwamba hakuna mwananchi atakayesumbuliwa kwenye kipindi chote cha
siku kuu.
“Niseme tu kwamba tumejipanga vya kutosha
kuhakikisha kila sehemu inakuwa salama na pia niwaombe watu kusherekea kwa
amani siku kuu ya pasaka na kwa Yule ambaye hataonekana kutaka kuvunja amani
sheria kali zitachukuliwa dhidi yake”Alisema Kamanda Mponjoli.
Kamanda Mponjoli pia amewata wazazi na walenzi kuwa
makini na watoto wao na kuhakikisha wanawachunga kwenye kipindi cha siku kuu huku
akipiga vita suala la disko toto.
Sanjali na hayo Kamanda Mponjoli, amewatahadharisha
watu ambao wamepanga kuandamana tarehe
26 april kuachana mara moja na suala hilo na kwamba wamejipanga vyema kulinda
amani ya Mkoa na mtu yeyote ambaye atabainika hatua kali zitachukuliwa dhidi
yake.
Post A Comment: