Raia
wawili wa Nchini China wamefariki Dunia wakati wakiwa ndani ya shimo lenye kina
cha Urefu wa zaidi ya mita 100 wakati wakifanya kazi ya kulipua miamba yenye
dhahabu mkoani Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa
polisi Mkoani Geita ,Mponjoli Mwabulambo, alisema
mnamo 20Mwezi wa tatu(3) saa tatu na dakika arobaini usiku, raia hao walifikwa na umauti wakiwa katika kijiji cha Nyamtondo ndani ya mgodi
unao milikiwa na Mayala Ngweso,
mfanyabiashara wa madini katika mgodi wenye PML No.0001333, ulio na ubia na
kampuni ya kichina iitwayo TAICHANGAIN TANZANIA
GROUP katika Kata ya Kaseme tarafa ya Butundwe wilaya na mkoa wa Geita.
Kamanda
ameeleza chanzo cha ajali hiyo ni uzembe uliofanyika na kupelekea kulipukiwa na
mlipuko wakati wakiwa ndani ya shimo na kusababisha majeraha makubwa kwenye
miili yao ambayo yalipelekea vifo vya raia hao.
Amewataja
Raia hao ambao ni Bw,Li-Shaobin,{44}, mwenye passipot No 6796105 ,ambae amepata
majeraha makubwa kisogoni, na Bwn,Qian Zhaorang, {49}, mwenye passipoti No 5834285,ambae amepata majeraha makubwa
kichwani na kuvunjika mguu wa kulia.
Amesema
miili yao imefanyiwa uchunguzi na daktari mnamo 24 machi mbele ya Shann Ly,{29} mwenye Paspoti No E.5968863 ambae ni
site Meneja, miili yao iliihidhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya
Makoye iliopo Geita.
Pia
ameongeza kwa kusema hawawezi kumshikilia mtu yoyote kutokana na ajali hii
kwani uchunguzi umeonesha chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wao na kutochukua
tahadhari kabala ya kuanza shughuli zao.
Kamanda
hiyo ametoa rai kwa wachimbaji wote kuchukua tahathari pale wanapofanya
shughuli za uchimbaji ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Post A Comment: