Wanafunzi wakishangilia baada ya kupatiwa madawati kutoka tigo.
Na Joel Maduka.
MKOA wa Geita umeendelea kuneemeka na misaada inayotolewa na wadau pamoja na mashirika mbalimbali katika kutatua changamoto za elimu, kampuni yaTIGO nayo imejitokeza na kutoa msaada wa madawati 185 yenye thamani ya Sh. Milioni 31.
Tigo ambayo ipo katika msimu wa fiesta 2016 ikiwa sambamba na kampuni ya Prime Time Promotion inayoandaa burudani hiyo kabambe, imeendelea kutoa misaada yake katika maeneo mbalimbali nchini.
Akisoma taarifa kwa Mkuu wa mkoa wa geita Meja jenerali Msataafu Ezekiel Kyunga, Meneja wa Tigo kanda ya ziwa Edgar Mapande alisema kuwa kapuni hiyo inatambua umuhimu wa elimu."Sisi kama tigo tunatambua umuhimu wa elimu na tumekuwa tukidhamini burudani mfano kwa mwaka huu fiesta na tumeona sio vyema kuendelea kudhamini burudani huku wanafunzi wakiendelea kukaa chini hivyo tumeonelea kwamba tuchangia kiasi hiki cha madawati ambacho kitagawiwa kwa shule ya msingi,mwatulole ambayo itapata madawati 50, kivukoni 45 ukombozi 45 na nyakumbu 45 mradi huu unadhihilisha nia yetu ya dhati ya kujenga mazingira ya kusomea"alisema Mapande.
bomba mbili,
Kutokana na msaada huo mkuu wa mkoa Ezekiel Kyunga amewashukuru wadahu ambao wameendelea kujitokeza kutoa michangango ya madawati na kusapoti elimu.
Kwa upande wao wanafunzi waliokuwepo shuleni hapo wameishukuru kampuni ya tigo na kuwaomba wadahu wengine kujitokeza kwa wingi kusapoti swala la elimu katika shule zilizopo Mkoani Geita.
Mkoa wa Geita umekusanaya zaidi ya Sh. Bilioni 1.7 kwa ajili ya madawati katika harambee iliyofanyika hivi karibuni, ambapo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Selemani Jafo alitaka michango inayotolewa na wadau ithaminiwe."michango iliyotokana hapa ni mikubwa mno na mimi niwashukuru wadahu wote ambao kwa pamoja hapa michango hii mmefanya harambee yetu itaingia katika rekodi ya harambee zilizofanyika"alisema Jafo.
Shule ya msingi mwatulole inawanafunzi 3300 na inajumla ya madawati 250 hivyo inaupungufu mkubwa madawati kulingangana na idadi ya wanafunzi.
|
Post A Comment: