Mwanafunzi abakwa na wanaume sita

Share it:









Mwanafunzi wa kidato cha tatu Sekondari Buseresere Wilaya ya Chato mkoani Geita, amebakwa na watu sita wanaodhaniwa kuwa ni wezi.

Akizungumza katika Kituo cha Afya Katoro ambako amelazwa kwa matibabu, mwanafunzi huyo alisema usiku wa kuamkia juzi akiwa amelala, alisikia mlango ukigongwa kwa nguvu na baadaye watu waliingia ndani hadi kwenye chumba alichokuwa amelala mama yake.

Alidai muda mfupi baadaye alisikia sauti ya mwanaume ikimtaka mama yake atoe fedha na kumlazimisha alale chini, lakini aliwajibu hakuwa na fedha.


“Nikiwa chumbani watu sita wakiwa na mapanga walisukuma mlango wangu na kuingia wakanilazimisha nivue nguo, huku wakinitishia panga nilipoanza kuvua wakanisukumia kitandani na kuniingilia mmoja baada ya mwingine,” alidai binti huyo huku akibubujikwa machozi.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Katoro, Peter Jange amesema mwanafunzi huyo ameingiliwa kimwili na kujeruhiwa.
Share it:

mapenzi

matukio

Post A Comment: