Makamu wa Rais wa UTPC,Jane Mihanji,akizungumza kumbukumbu ya Mwangosi.
Ikiwa Leo ni Kumbukumbu ya miaka 5 tangu kufariki kwa mwanahabari Daudi Mwangosi, Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa wakati akitekeleza majukumu yake.
Mwaka huu UTPC imeungana na wanahabari wa mkoa wa Mwanza katika kumbukumbu ya kifo cha Daud Mwangosi kwa kufanya mkutano na vyombo vya habari.
Akiongea katika mkutano huo makamu wa Rais wa UTPC Bi. Jane Mihanji alisema kuwa, viitendo vya kuwapiga, kuwanyanyasa, kuwaharibia vifaa vya kazi na kuwauwa waandishi wa habari ni vitendo visivyovumilika katika tasnina ya habari na kwa namna moja au nyingine vinaminya uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Alitoa wito kwa waandishi wa habari kote nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uweledi na kuzingatia maadili ya kazi na taaluma ya uandishi wa habari .
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, amebainisha kwamba
tunzo ya Daudi Mwangosi mwaka huu pia haikupata mshindi kwa namna ambavyo jopo
la tuzo hiyo lilivyoweka vigezo vyake ikiwemo Mwandishi anayepaswa kuichukua
awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini. Mwaka 2013 tuzo hiyo
ilichukuliwa na Mwanahabari Absolum Kibanda.
|
Post A Comment: