Wajasilia mali Mkoani Geita watakiwa kutumia furusa zilizpo Mkoani humo.

Share it:

Akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi,katibu tawala wa wilaya Thomas Dimme akitoa neone la kwa  wajasilia mali.


 Peter Kingu ni mkuu wa kitengo cha wajasilia mali mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha (FSDT)akimkuaribisha mgeni rasimi kuongea na wajasilia 

Akifafanua jambo na waandishi wa habari.

Methew Masele ambae ni mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa wa Geita,akizungumzia furusa zilizopo Mkoani Geita.

Meneja Mradi wa TPSF Celestine Mkama,akitoa maelekezo kwa wanasemina


Denis Kisoka mkufunzi mkuu wa mafunzo ya wajasilia mali ,akielezea njia tatu za namna ya kuinua kipato na mtaji.


Elizabeth Bigambo mjasilia mali wa mgahawa,akichangia mawazo ya namna ya kuinua kipato.


wajasilia mali wakifatilia kwa makini mafunzo.

Mgeni rasimi akiondoka katika eneo la semina.


Wajasilia mali mkoani Geita ,wamenufaika na mafunzo yaliyotolewa na sekta binafsi Tanzania (TPSF) ikishirikiana na mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania (FSDT)  huku wakiamini kuwa mafunzo hayo yamewapa ujuzi wa kuimalisha biashara zao na uendeshaji wa biashara. 


Mafunzo hayo yamedumu kwa siku mbili yalianza jana tarehe 1 na yamemalizika leo tarehe 2 huku wafanyabiashara hao wadogo wakinufaika na namna ambavyo wanawez kuendeleza mitaji mikubwa na kuinua vipato zaidi.

Akimwakilisha mgeni rasimi ambae ni mkuu wa wilaya ya geita katika mafunzo hayo,katibu tawala wa wilaya ya Geita,Thomas Dimme amewataka wajasilia mali kutumia furusa zilizopo mkoani Geita ambazo zitawasaidia kuinua vipato vyao.

aidha kwa upande wao wajasilia mali ambao wamejitokeza katika mafunzo hayo,Rasta Ikolongo Otoo,alisema kuwa ni vyema kwa taasisi ambazo zimekuwa zikitoa mafunzo ya kuwasaidia wajasilia mali kuwasaidia kupata mikopo."Mikopo imekuwa ni shida kwa wajasilia mali na baadhi ya mashirika na makapuni yameshindwa kuwasaidia wajasilia mali wadogo hali ambayo inasababisha maisha yao kuwa chini.alisema Otoo.

Kwa upande Meneja Mradi wa TPSF Celestine Mkama,alisema kuwa wataendelea kutoa mafunzo na pia wataakikisha kwamba wanaongeza nguvu ya kuwafikia na wale ambao wapo nje ya miji ambao wapo vijijini ili na wao waweze kuwa na elimu ya ujasilia mali ambayo itawasaidia katika maisha yao.

Share it:

matukio

Post A Comment: