Ni kibao kilichopo katika chuo cha Rich Rice kikikukaribisha chuoni hapo.
Wanachuo wakiwa katika hali ya mgomo wa kuto kuingia madarasani . |
Wanachuo wakielekea kwenye Hostel . |
Makamo mkuu wa chuo hicho Elisha Ndelembi akitoa maelezo kwa wanahabari juu ya hatua ya kugoma wanafunzi. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akitoa maelekezo mbele ya wanafunzi. |
Wanachuo wakifatilia kwa makini maagizo ya Mkuu wa Wilaya. |
Na Joel Maduka
Wanafunzi wa chuo cha uwalimu cha
RICH LISE kilichopo mkoani Geita,wamegoma kuingia madarasani kwa kile
kinachodaiwa ni kufutwa kwa kozi ya uwalimu wa cheke chekea ,hali ambayo
imewasababisha kushindwa kujua mwafaka wao kwani ni muda sasa tangu waanze
masomo chuoni hapo na taarifa hiyo imekuja muda ambao walikuwa hawadhani
kutokea kwa jambo kama hilo na kusababisha kuwa na mshituko
Happynes Charles,ni mwanafunzi
wa chuo hicho,alisema kuwa kero hizo zimewachosha kwani walimu wamekuwa
wakiwazungusha na kushindwa kujua mwafaka wao ni nini”kiini cha kugoma jana
mkurugenzi alitutangazia kwamba kozi tunayoisoma sisi haipo na kwamba wanafunzi
wote hatujasajiliwa kwa hiyo ndio maana leo tumetaka kujua mwaka wetu kama
tumesajiliwa au la lakini tunashukuru
tumejua ukweli wetu kwamba hatuna chetu hapa”alisema Happynes.
Hata hivyo sifa ya wanafunzi wa uwalimu ni kuanzia kuwa na ngazi
ya divitioni three,na wengi ambao wanalalamika kutokujua haki yao ya msingi ni
wale ambao wana division four,Betrice Zakayo yeye ni mwanafunzi wa chuo hicho
ambapo alisema kuwa yeye ni bora wapatiwe fedha zao waondoke huku akiomba
serikali kuingilia kati swala hilo.”Mimi nina three lakini sitaki kusoma hapa
masomo yanaanza mwezi wa kumi lakini sisi tuliambiwa tulipoti mwezi wa nane na
hera zimeliwa zote na alikula hera ameondoka
turudishiwe pesa zetu zirudi kama mambo
hayaeleweki twende vyuo vingine”alisema
Beatrice.
Makamo wa chuo hicho,Bw,Elisha Ndelembi,alisema
waliondoka kwenda nectar mwanza kwa lengo la kujua program hiyo”jambo hili
ambalo limekuwa likienea sana Kwamba ECD
yani program hii wanayoendelea nay o wanachuo haijasajiliwa na muda wake
umepita ilikuwa ni uko nyuma mwisho wake
ni 2015 basi tumekwenda tukakuta uwongozi wa necta kanda uko vizuri ukawa wazi
sana wakasema kwamba tunasikitika mno na mmefanya vizuri kuja kwani hiyo ECD
imeshafutwa na tulikuwa na mpango wa kuja kukifungia chuo hicho”alisema
Ndelembi.
Mkuu wa wiaya ya Geita,Herman
Kapufi amewataka wanafunzi hao kuwa watulivu huku akiagiza wakuu wa necta kufika
chuoni hapo, afisa taaluma na afisa
elimu kufika saa tatu ili kutatua
changamoto zilizopo chuoni hapo.huku akiagiza idara ya uhasibu kuwa na
kumbukumbu zote za malipo ya wanafunzi hao.
Post A Comment: