CHADEMA KUFANYA MAANDAMANO KUSHINIKIZA MAGWANGALA KUACHIWA WILAYANI GEITA.

Share it:

Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Geita ,Muhere Mwita akifafanua juu ya uwamuzi wa chadema kudai mangwangala mbele ya waandishi wa habari.



GEITA:Chama cha Demokrasia na maendeleo chadema Wilayani Geita,kimesema kitafanya maandamano kushinikiza swala la kumwagwa kwa miamba taka ya dhahabu(mangwangala) kutokana na kwamba muda mrefu umepita tangu agizo la Rais John Magufuli alilolitoa kwa wiki tatu kuwa maeneo yawe yamepatikana na mangwangala yaanze kumwangwa.

Kauli hiyo imesemwa na mwenyekiti wa Baraza la vijana  chadema Wilayani hapa,Muhere Mwita wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,alisema kuwa swala hilo limeonekana kama ni kuwahada wananchi kwani vijana wengi wamechangia gharama kwa kuunda vikundi ambavyo waliamini kuwa ndani ya muda mfupi ambao agizo kutolewa na  Rais swala hilo lingekuwa limetekelezwa.

“Vijana walimwomba Mh, Rais awapatie magwangala kwenye mkutano wa wananchi Geita mjini,ambapo tamko lilikuwa ni ndani ya wiki tatu yawe yametolewa na kwamba vijana watengeneze vikundi lakini tunaona serikali ya wilaya na Mkoa hawajatoa maelezo yoyote na hatima ya swala la magwangala,mimi ni na laani kitendo hicho na kwamba sisi kama umoja wa vijana chadema tupo tayari kuandamana muda wowote na siku yoyote kwenda kwa Mkuu wa wilaya kujua hatima ya magwangala”alisema Mwita.

Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi,alisema kuwa kuna maswala mamchache ambayo walikuwa wanakamilisha ili waweze kutoa magwangala lakini kutokana na kwamba kuna baadhi ya maeneo ni sehemu ambayo kuna misitu nauwezi kukata mistu paka  kibali kutoka wizara ya mali asili na utalii.

Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi.

“Tumekwisha andika barua na watu wamekwisha kwenda Dodoma kumwona waziri mwenye dhamana  ili aweze kutoa kibali cha kuruhusu baadhi ya miti kukatwa hili kusafisha njia ya mangwangala swala la wananchi kuandamana ni utaraibu wa fujo ”alisema Kapufi.

Agizo la utowaji wa magwangala lilitolewa tarehe 31 mwezi wa nane ,Rais John Pombe Magufuli alitoa maelekezo ya wananchi kupatiwa ndani ya wiki tatu na sehemu ziwe zimepatikana.


Imeandaliwa na Joel Maduka.
Share it:

habari

Post A Comment: