NAHODHA WA YANGA,NADIR CANAVARO.
|
Nahodha wa mabingwa
watetezi Yanga,Nadir Haroun ‘Canavaro’ametamba kuwa hakuna namna lazima wapate
pointi sita katika Ardhi ya Shinyanga na kuanza na mchezo wa Kesho dhidi ya
matajiri wa Mwadui uwanja wa Kambarage Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Canavaro amesema kuwa ni dhambi kuilinganisha
Mwadui na sisi kwani tumeweze kucheza na timu kubwa Afrika kuliko hii timu ya
Kocha mwenye maneno mengi najua kesho baada ya kumshushia kichapo atakuwa na
visingizio vingi hivyo tumejipanga kushinda mchezo wetu dhidi ya Mwadui.
“Mchezo wetu na
Mwadui utakuwa kama fainali kwetu na tutacheza kufa na kupona ili tuweze
kuondoka na pointi tatu kwani msimu uliopita tulitoka nao sare kutokana na
uwanja kuwa ulikuwa na maji hivyo kipindi hiki hakuna Mvua japo uwanja si
rafiki ndio maana tumejipanga ukizingatia tulikuwa tunafanya mazoezi katika
uwanja wa Kaunda sababu ni mbovu kama wa Kambarage”alisema Canavaro.
Aidha Canavaro
amesema kuwa hata kocha Mkuu Hans Van Der Pluijm amewapa mbinu za kucheza
viwanja vya mikoani na pia ameshayafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika
mchezo wetu ambao tulicheza ugenini na Ndanda tulilazimishwa sare ya bila
kufungana hivyo tunashukuru baadhi ya wachezaji wetu wamerudi ambao
walikosekana katika michezo yetu miwili.
Yanga wanategemea
kucheza na Mwadui mchezo unaotabiriwa kuwa na upinzani wa aina yake kutokana na
matajiri hao wa Mwadui wanafundishwa na Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelu Julio ambaye
ni mwanachama wa Simba hivyo inatafasiriwa kuwa yeye ana mapenzi na Simba na
atawakazia Yanga kuibuka na ushindi siku ya kesho.
TAZAMA MECHI NYINGINE AMBAZO
ZITACHEZWA WIKENDI HII.
JUMAMOSI SEPTEMBA 17:
.Mwadui FC vs Yanga
.Mbeya City vs Prisons
.Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar
.Azam FC vs Simba
.Ruvu Shooting vs Mbao FC
.Majimaji vs Ndanda FC.
JUMAPILI SEPTEMBA 18:
.African Lyon vs Toto African
.Stand United vs Jkt Ruvu.
Post A Comment: