Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisisitiza juu ya kutokukubaliana na baadhi ya matajiri kuendelea kuwaonea wasio na uwezo wa kifedha. |
Mtu mwenye ulemavu wa miguu, Kamuli Shilinde(30) ambaye ni mkazi wa kijiji na kata ya Rwamgasa Wilayani
na Mkoani Geita amemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl, Heriman Kapufi kumsaidia
kulipwa malipo yake kiasi cha shilingi laki tano(500,000) alizodhurumiwa na
mwekezaji wa Madini mzawa
Emannuli Gambi ikiwa ni malipo baada ya kuajiriwa.
Aidha Shilinde ametoa kilio
chake hicho mbele ya mkuu huyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
uwanja wa kituo cha polisi uliokuwa na lengo la kuhimiza wananchi kuchangia maendeleo na kusikiliza
kero zao .
Pia mtu huyo mwenye ulemavu
ameendelea kusema kuwa tajiri huyo ambaye ni mkazi wa Geita mjini
alimuajiri kuwasachi wachimbaji wadogo wanaotoka
kwenye maduara yake ili wasiweze kutoka na dhahabu na kutokomea nazo.
“Mkuu wa Wilaya mimi nashukuru sana ujio wako kwenye kata yetu ya
Rwamgasa mimi ni mlemavu kama unavyoniona lakini ni muhanga niliyedhurumiwa
pesa zangu na tajiri wa madini anaitwa Emannuel Gambi kila ninapomtafuta natishiwa kufungwa naomba msaada wako anilipe
pesa zangu ninazomdai” alisema Shilinde
“Nikuwa nafanya kazi ngumu sana mkuu wangu jua na mvua vilikuwa
vyangu na kibaya zaidi nilikosana na wachimbaji niliokuwa nikiwasachi mifukoni
mwao nilifanya kazi hiyo kwa uadilifu na uaminifu mkubwa sana bira yeye kupata shoti hata kidogo lakini alimbikiza pesa zangu na
nilipoanza kudai nilikuwa natishiwa kufungwa naomba msaada mkuu wangu”aliongeza
Shilinde.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl Herman Kapufi amehaidi kulifuatilia swala
hilo kwa tajiri huyo na kwamba hatokubali kuona wananchi kwenye Wilaya
yake wadhurumiwa na
watu wenye fedha na kwamba kama kuna wawekezaji wanawaza kuja kuwekeza na
kuwadhurumu wezao kwa kutumia fedha zao watafute pa kwenda huku akimtaka mlemvu
huyo kumpigia simu siku ya jumatatu.
“Nimepokea malalamiko yako ndugu yangu lakini nakuahidi
kulifatilia mara moja na utalipwa fedha zako mara moja kwani hakuna mtu yeyote
aliyeko juu ya sheria nitakuachia fedha kwa ajili ya kunipigia simu yangu ya
mkononi na huyo tajiri nitamchukulia hatua za kisheria”alisema Kapufi
Alipotafutwa tajiri huyo kwa njia ya simu yake ya mkononi alimtaka
mwandishi wa habari hii kuandika chochote alichokisikia kutoka kwa mlemavu huyo
huku akisema yeye hawezi kudaiwa na mtu kama huyo na kwamba hawezi kutoa ajira
kwa mtu mlemvu wa viungo kisha kukata simu na kuzima.
“Andika chochote ama lolote ulilosikia akisema yeye mlemavu huyo kwenye mkutano huo wa hadhara mimi kwa uwezo nilionao siwezi kutoa ajira kwa mlemvu na
sijawahi kudaiwa na mlemvu kwanza mimi simjui”alisema tajiri huyo.
Post A Comment: