Klabuya Lipuli ya mkoani Iringa
imetamba kuwa itahakikisha inaanza kwa ushindi dhidi ya African Sports
‘Wanakimanumanu’mchezo wa daraja la kwanza inayotarajia kuanza Septemba 24
mwaka huu ambako watawakalibisha vijana wa Tanga.
Akizungumza juu ya hatima
hiyo,Mratibu wa Mazoezi na pia ni Msimamizi wa Usajili,Haruna Saleh,amesema
kuwa wamejianda kuanza vizuri msimu huu katika Ligi hiyo kwani wamefanya
maandalizi ya kutosha na kambi yao waliifanyia Dar es salaam katika uwanja wa
Karume wakiwa chini ya Kocha Mkuu Richard Amache anayekinoa kikosi hicho.
“Kilichobaki ni kuwaomba
mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa kuja kuwapa hamasa ya
ushindi wachezaji wao ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuipandisha Ligi
Kuu msimu ujao kwani wanaamini ligi itakuwa ngumu kwa kila timu kutaka kupanda
Ligi”alisema Saleh
Lipuli wataanza kampeni
yao ya kutaka kupanda Ligi kwa kuwakaribisha Wana kimanumanu ambao msimu uliopita
waliweza kushuka daraja kutokana kuwa na migogoro ya Uongozi na kupelekea timu
tatu za Tanga kuweka rekodi Dunia kwa kushuka kwa pamoja ambazo zilikuwa ni
African Sports,JKT Mgambo na Coastal Union.
Hata hivyo Uongozi wa timu
hiyo wanajivunia kuwa na wachezaji vijana ambao watasaidiana na wakongwe na
uwepo wa mchezaji mkongwe wa zamani wa Simba Salum Machaku,utawapa hamasa ya
kufanya vizuri katika michuano hiyo kwani ana uzoefu wa kutosha na soka la
Tanzania.
Post A Comment: