|
Mifano ya mashimo ya vyoo bora |
|
Vyoo bora kikiwemo choo ambacho mlemavu anaweza kukitumia kwa wepesi zaidi. |
|
Mfano wa choo Bora kilichokamilika. |
|
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ali Kidwaka akipewa maelezo na mtaalam wa ujenzi wa vyoo bora. |
|
Maelezo kutoka kwa wataalam tofauti juu ya ubora wa vyoo yakiendelea. |
|
Mwandishi wa habari wa ITV,Rose Mweko akinawa mikono baada kutoka chooni. |
|
Rose Mweko akitoka chooni. |
|
Dr Hamis Marebo akimkaribisha Mgeni rasimi kuzungumza na wananchi juu ya swala matumizi ya vyoo na kunawa maji pindi wanapotoka chooni. |
|
Muonekano wa baadhi ya vyoo visivyo bora. |
|
Moja kati ya vyoo duni. |
|
Dr Marebo akiangalia choo ambacho kimekoswa maitaji madogo kukifanya kiwe Bora |
|
Mtafiti wa Taasisi ya magonjwa ya
binadamu Bi, Yolanda Mbatia,Akimkabidhi mkurugenzi hati ya kituo kilichozinduliwa cha mafunzio ya vyoo bora |
|
Ali Kidwaka,akionesha mfano ambavyo wananchi wanatakiwa kufanya pindi wanapotoka chooni. |
|
Mkurugenzi Kidwaka akifafanua jambo kwa wananchi. |
|
Dr Marebo akitoa Elimu kwa wananchi namna wanavyotakiwa kuwa mabarozi wema katika matumizi sahihi ya vyoo. |
|
Mtafiti wa Taasisi ya magonjwa ya
binadamu Bi, Yolanda Mbatia,Akielezea mafanikio waliyoyapata tangu kuanzishwa mradi wa vyoo bora. |
GEITA:Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya Geita,wametakiwa kuwa na mwitikio wa kutumia vyoo bora na kunawa mikono wakati wote pindi wanapotoka Chooni.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya,Ali Kidwaka wakati wa zoezi la kukabidhiwa kituo cha mafunzo ya vyoo bora katika kata ya Katoma .
Kidwaka
,amesema kuwa tangu mwaka 2014 matumizi ya kutumia vyoo bora na kufata na
unawaji wa mikono kwa wananchi pindi wanapotoka chooni asilimia zimeongezeka hadi kufikia 67 paka
asilimia tisini ya sasa na bado jitihada zinaendelea kufanyika katika
kuakikisha wananchi wanatumia vyoo bora ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko
ambayo yanaweza kutokea kutokana na kutokutilia maanani matumizi sahihi ya
vyoo.
“Tunatambua
kuwa matumizi sahihi ya vyoo ni muhimu kwa kila mwananchi ili kuepukana na
magonjwa ambayo yanaweza kutishia kuondoa uhai wetu hivyo ni vyema kwa kila
familia kuwa na choo bora na kukitumia.”alisema Kidwaka.
kwa upande wake, mtafiti wa Taasisi ya
magonjwa ya binadamu Bi, Yolanda
Mbatia,amesema kuwa lengo la kuja kuzindua mradio huo wa vyoo bora ni kutokana
na hapo nyuma katika kata hiyo watu wengi walikuwa wanapata magonjwa
yanayotokana na kinyesi cha binadamu.
Afisa
afya wa wilaya ya Geita,Nesfori Sungu,amesema
kuwa kulingana na maelekezo ya mkuu wa wilaya kila mwananchi anatakiwa kuwa na
choo ifikapo tarehe 30 mwezi wa Tisa.
“Ni kila
mwananchi anatakiwa kuwa na choo bora na
ifikapo tarehe 30 mwezi huu kama ambavyo mkuu wa wilaya alivyoagiza.”alisema
Sungu
.
Hata
hivyo wananchi wa kata ya Katoma
wameiomba serikali kupitia mradi wa vyoo bora kuona uwezekano wa kupunguza
gharama za utengenezaji wa vyoo hivyo.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
Post A Comment: