GEITA:Halmashauri
Ya Mbogwe Yafunga Mkataba Wa Ujenzi Wa Ofisi Makao Makuu Mapya.
Halmashauri Ya
Wilaya Ya Mbogwe Mkoani Geita Imeingia Mkataba Wa Ujenzi Wa Jengo La Ofisi Za
Halmashuri Zinazotarajiwa Kujengwa
Katika Kijiji Cha Bwelwa Kata Ya Mbogwe.
Halmashauri Imesaini
Mkataba Huo Na Kampuni Ya M/S C.F
Builders L.T.D Ya Jijini Mwanza .Mkataba Huo Utatekelezwa Kwa
Miaka Mitatu 2016/2019 Na Utagharimu
3,994,947,386.10
Akiongea Wakati Wa Kusaini Mkataba Huo Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Elias
Kayandabila Alisema Wamefikia Hatua
Nzuri Na Ujenzi Utaanza Muda Wowote Na Itakuwa Fursa Kwa Wakazi Wa Mbogwe
Kupata Ajira Za Muda Mfupi.
Vile Vile
Mkurugenzi Kayandabila Amesema Ujenzi
Huo Utajengwa Kwa Awamu Kutokana Na Upatikanaji Wa Fedha Na Ameiomba Serikali
Kuu Kuipa Kipao Mbele Halmashauri Kwa Kuwa Ofisi Zinazotumika Kwa Sasa Haziko
Rafiki Kiutendaji Kwani Mazingira Yamechakaa Na Hayatoshelezi Wtumishi Wote.
Diwani Wa
Kata Ya Mbogwe Sizya Nsika Amesema Amefurahi Kwa Hatua Iliyofikiwa Ya Kutia
Saini Kwani Jambo Hilo Amelisubiri Kwa Muda Mrefu Lakini Utekelezaji Wake
Ulikuwa Unalegalega .
Sizya Ametoa
Shukrani Za Pekee Kwa Mkurugenzi Mtendaji Elias Kayandabila Kwa Kutilia Mkazo
Suala Hili Muhimu.
Ujenzi Unaoenda
Kuanza Utapelekea Viwanja Vya Halmashauri Vilivyopimwa Kuuzika Baada Ya Kukosa Wateja Kwa Muda
Mrefu.Viwanja Hivi Vilipimwa Kwa Mkopo Kwa Makubaliano Vikiuzika Mkandarasi
Atalipwa Lakini Ilishindikana Baada Ya Wateja Kukosekana Na Kuingiza
Halmashauri Katika Mgogoro Na Mkandarasi.
Ujenzi Huu
Unarudisha Matumaini Kuwa Viwanja Vitauzika Sasa Kwani Watu Wengi Walikuwa
Wanasubiri Ujenzi Kuanza Ili Kujiaminisha Kuwa Makao Makuu Ya Wilaya Ya Mbogwe
Yatakuwa Mbogwe.
Imeandaliwa Na
Peter Makunga
Post A Comment: