Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ina idadi ya wazee wapatao 5704 Huduma ya Afya kwa wazee hao bado ni changamoto pamoja na Sera ya Serikali ya kuhakikisha wazee waliofikisha umri wa miaka 60 nakuendelea wanatibiwa bure katika hospital zote Nchini.
Hayo yalibainishwa
jana kwenye kikao cha wazee na wadau wa afya ustawi wa jamii na waandishi wa
habari wilayni Bukombe mkoani Geita.
Mzee
Radslaus Mgalula , bibi Getruda Sizya na
Mzee Enock Bugumba waliwaeleza wadau
kuwa pamoja na jitihada za serikali kuwatambua wazee kuhusiana na huduma za
matibabu bado Changamoto zinazowakabiri wazee hao ni pamoja na uhaba wa dawa,
umbali wa kufikia huduma hizo.
Wamesema zipo changamoto za vyumba vya huduma
havitoshi ,wazee kutokuthaminiwa na hivyo wanamuomba mh Rais Magufuli kupitia
waziri wake wa afya awatazame kwa jicho la huruma kwani bado wanateseka
hospitalini hakuna dawa.
Wazee
hao walisema wanakalishwa kwa muda mrefu kwenye foleni pia
wanaomba nao waingizwe kwenye mpango wa kufuatwa na gari la wagonjwa kama mama
mjamzito afatwapo huko kijijini kwani nao nguvu zimewaishia.
Afisa ustawi
wa jamii Wilayani humo,Amon Kafiriti alisema kuwa idara yake imejipanga kutoa
elimu ya kuwalinda wazee ili jamii hiepukane na imani za ushirikina
zinazopelekea kuwaua wazee kwa kuwakata
mapanga kwa kisingizio cha uchawi.
Aidha mganga
aneyehudumia chumba maalumu cha wazee katika hospital ya wilaya Dr Kabula Mwigulu amekili kuwa changamoto
hizo kwa wazee zipo ni kutokana na ufinyu wa bajeti fedha za kununulia dawa na
vifaa tiba hazitoshi sambamba na uhaba
wa miundo mbini ya majengo hayatoshi ndiyo maana sehemu nyingi wazee
wanataabika.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe Nikas Safari ametoa wito kwa wananchi kuchangia elfu 10 kila
kaya ili zipatikane fedha ambazo itakuwa jawabu la changamoto zinazowakabiri
wazee.
Safari alisema
wananchi waliopo Bukombe wapatao laki mbili wakichangia hiyo fedha dawa ,vifaa
tba miundo mbinu katika zahanati ,hasptal vitapatikana.
Hivyo
aliwahamasisha waheshimiwa madiwani wakasimamamie ujenzi haraka wa zahanati
kila kijiji ili kuondoa tatizo la kupata huduma mbali .
Imeandaliwa
na Peter Makunga.
Post A Comment: