Meneja mahusiano ya jamii wa GGM,Manase Ndoloma akiteta na wananchi ambao wameathirika na sumu ya sayanaidi wakiwa kwenye zahanati ya Busanda. |
Wananchi wakiendelea kusubilia kupatiwa huduma ya kwanza kutokana na kulamba na kunusa sumu hiyo. |
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Busanda,Steven Masesa akifafanua jambo na namna ambavyo wao kama zahanti wamefanikisha kutoa huduma. |
Mgonjwa akiwa amezidiwa akiwa nje amelala. |
Mtaalam wa maswala ya uokoaji kutoka kampuni ya GGM ,Paul Kagondi akitoa elimu namna ambavyo wananchi wanaweza wakajikinga ili wasiathirike na sumu ya sayonaidi. |
Mtaalam akionesha kifaa cha kukagulia sumu hiyo. |
Mtaalam akikagua na kuonesha sumu hiyo ambayo imeonekana maeneo ya kijiji cha Busanda ikiwa imetapakaa. |
Wataalam wakiendelea na ukaguzi katika maeneo ya kijiji cha Busanda. |
GEITA:Kampuni
ya uchimbaji wa madini Mkoani Geita (GGM) Imepeleka wataalam na madaktari
katika kijiji na kata ya Busanda Wilayani Geita lengo likiwa ni kutoa huduma
kwa waathirika wa sumu ya sayanadi.
Siku
ya jumapili September 11 ,Mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Simomo Waziri(
4) alifariki dunia na huku mifugo 30 ikipoteza maisha baada ya kulamba kitu
kinachosadikika kuwa ni sumu ya sayonidi
iliokuwa ikisafilishwa kwa usafiri
bodaboda bira kuhifadhiwa vizuri.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Meneja
Mausiano ya jamii wa mgodi wa GGM Manase Ndoloma Alisema wameamua kupeleka
wataalam na madokta ili kuwasaidia
waathirika nah ii ni kutokana ma mahusiano mazuri waliyonayo na wananchi
wanaouzunguka mgodi.
“Sisi kama mgodi ambao tupo Mkoani hapa
tuliguswa na tukio hili baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari na kwasababu
ni swala ambalo lipo ndani ya uwezo wetu ndio maana tumeamua kutuma wataala na
kusaidia tatizo hili.”alisema Ndoloma.
Baadhi ya waathirika wengi wao wakiwa ni watoto wadogo walikuwa wamekusanyika katika zahanati ya Busanda walieleza madhara
walioyapata baada ya kunusa na kulamba sumu hiyo kuwa wamekuwa wakijisikia
tumbo kuuma na kizunguzungu kikali .
.
Mtaalam
wa maswala ya sumu ya Sayanaidi kutoka ndani ya Mgodi huo Paul Kagondi amekili kuwepo kwa sumu hiyo ya Sayanaidi katika eneo
hilo na kwamba wameshafanya uchunguzi na kuakikisha wanatatua tatizo ambalo
limetokea kijijini hapo.
“Tumefika
kijijini hapa na tumefanya uchunguzi na kubaini kweli kulikuwa na sumu hiyo
lakini tumeshafanya uchunguzi na kutatua tatizo la sumu hiyo ambayo ilikuwa
imesambaa”alisema Kagondi.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
Post A Comment: