Mzee Didas Shitobero,Akionesha eneo ambalo limechimbuliwa na kutolewa kichanga hicho. |
Mzee Didas Shitobero,akielezea namna tukio lilivyokuwa. |
Akiwa na jirani yake wa karibu . |
Haya ni makazi ya kwa Mzee Didas Shitobero. |
Mwenyekiti wa kitongoji ,Mathias Bumbuli akielezea namna alivyoguswa na tukio hilo |
GEITA :Katika
hali isiyo ya kawaida familia ya mzee Didasi Shitobero, wa kijiji na kata Bugulula ,Wilayani na Mkoani Geita,wamejikuta
wakiingiwa na hofu kubwa kutokana na
kukutwa kitoto kichanga cha siku moja
kilichozaliwa kikiwa kimefariki kimefukuliwa
nyuma ya nyumba yake.
Maduka
online imefika kijiji hapo na kujionea kaburi la mtoto huyo wa siku moja likiwa
limefukuliwa na mwili kutolewa ndani ya kaburi hilo.
Baba wa
familia hiyo, Didasi Shitobero alisema kuwa tukio hilo lilitokea jumatatu ambapo baada
ya kuamka siku hiyo walikuta kaburi la mtoto likiwa limefukuliwa na mwili
hakuwemo katika kaburi hilo.
“Tumesikitishwa
sana na kitendo hiki cha kufukuliwa kwa mtoto mchanga kwani tumeshindwa kujua
ni nani ambae amefanya kitendo cha namna hii ambacho ni cha kinyama
kabisa”alisema Shitobero.
Kutokana na
tukio hili kuwasitajabisha baadhi ya majirani kwa kufukuriwa kwa kichanga hicho
walisema kuwa wale wote ambao wamekuwa
na tabia za namna hiyo ni vyema wakaachana nazo kwani imani hizo sio nzuri.
Kutokana na
ukubwa wa swala hili madukaonline ilibidi
imtafute mwenyekiti wa zengo Mathias Bumbuli,alisema ni vyema kwa jamii iliyopo
katika eneo ambalo analiongoza wakaachana na maswala ya imani za kishirikina
kwani hakuna faida yoyote ambayo mtu anaweza kupata kwa kufanya maswala hayo.
Post A Comment: