Kikosi kikiwa katika utulivu. |
Kikosi cha Kilimanjaro Queen kikiwa katika mazoezi. |
Timu ya Tanzania bara ya Wanawake Kilimanjaro Queen,imeanza
maandaliza ya CECAFA kwa kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Timu ya Wanawake
wa Burundi mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
jana.
Akizungumza kwa njia ya simu ,Kocha Mkuu wa
timu hiyo,Sebastian Nkoma,amesema kuwa kweli nimeweza kupata ushindi wa magoli
matatu katika mchezo wangu wa kwanza nikiwa na timu hiyo japo kuwa mchezo
haukuwa rahisi ila vijana wangu wananipa matumaini ya kufanya vizuri michuano
ya wanawake yanayotarajia kuanza Septemba 11,mwaka huu nchini Uganda.
“Unajua kama timu mnaanza kwa ushindi tena timu kubwa kama
Burundi ambayo nayo inashiriki michuano hiyo ni dalili njema kuwa tutakuja na
ubingwa kwani tunaenda kupigana mwanzo mwisho ila tunajua tupo kundi ngumu
ambalo linajumuisha Ethiopia na Rwanda hivyo tunawaomba watanzania watuombee
tufanye vizuri”alisema Nkoma
Kilimanjaro Queens ilipata magoli yake dhidi ya Burundi kwa
kupitia wachezaji wake mahiri Asha Rashid,Mwanahamis Omary “Gaucho’ na moja
wakijifunga kutokana na piga ni kupige katika lango lao na Timu hizo mbili
zinatarajia kuondoka Leo Bukoba na kuelekea nchini Uganda kwa michuano hiyo
inayotarajia kuanza siku ya Jumapili.
Michuano hii kwa upande wa Wanawake ni kwa mara ya kwanza
inaanzishwa katika ukanda huu wa CECAFA hivyo ni fursa kwa timu za wanawake
kufanya vizuri na kujimarisha katika mashindano ya CAF na zimegawanywa katika
makundi mawili.
Kundi A:
Kundi B:
.Kenya
Kilimanjaro Queens.
.Uganda
Rwanda.
.Burundi
Ethiopia
.Zanzibar
Kilimanjaro Queens inatarajia kutupa karata yake ya kwanza
Septemba 12 kucheza na Rwanda kabla ya kumalizana na Ethiopia Septemba 16 na
Zanzibar wao wataanza na Burundi Septemba 11 na wenyeji nao watacheza na Kenya
siku hiyo hiyo.
Post A Comment: