MAREKANI YASHAMBULIA AL-SHABAB SOMALIA

Share it:

Marekani imefanya mashambulizi mawili ya anga kusini mwa Somalia mapema wiki hii ambayo yaliwaua wanamgambo wanne wa Al shababu kundi lenye ushirikiano na Al-Qaida.
Komandi ya Marekani barani Afrika imesema mashambulizi ya Jumatatu yalikuwa ni kujibu shambulizi lililofanywa na kundi kubwa la wapiganaji wa Al-Shabab waliokuwa na silaha katika operesheni ya pamoja ya kupambana na ugaidi baina ya Marekani na Somalia.
Jeshi la Marekani limewahi kutumia ndege zisizo na rubani kulenga viongozi waandamizi wa Al-Shabab.
Pentagon ilisema mwezi Juni kwamba mwishoni mwa mwezi mei kulifanyika shambulizi dhidi ya Abdullahi Haji Daud, mmoja wa wapanga mipango waandamizi wa kijeshi wa Al-Shabab.
Kiongozi huyo wa Al-Shabab alihudumu kama mratibu mkuu wa mashambulizi ndani ya Somalia, Kenya na Uganda.
Chanzo VOA SWAHILI.

Share it:

habari

Post A Comment: