Mkuu wa wilaya ya Mbongwe Martha Mkupasi akifafanua juu ya mafunzo ya madereva boda boda. |
Boda boda kazini.
Serikali Wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita imeanza
kuwatambua vijana wanaojiajili
hususani waendesha Bodaboda kwa
kuwapa Elimu itakayowawezesha kupokea na kuzitumia
Fulsa mbalimbali zitolewazo kwa vijana.
Akizungumza
na Maduka online Mkuu wilaya ya Mbogwe Martha
Mkupasi alisema wamekuwasudia kutoa elimu kwa waendesha boda boda kutokana na
kwamba hawana mabasi ya kutosha.
“elimu ambayo tunatoa ni
vyema wakajiunga kwenye vikundi ili tuweze kuwatambua na halmashauri itasaidia
kuwasajili vijana hao”alisema Mkupasi.
Hatua ya Serikali
wilayani hapa kuwapatia elimu vijana hao waendesha Boda boda ni kutokana na
uelewa wao mdogo hali ambayo wamekuwa wakikimbizana na Polisi sanjari na kukosa
sifa za kuaminiwa na kutambuliwa.
Mkupasi ametoa wito kwa jamii kutambua kuwa boda boda ni ajira
inayosaidia vijana wengi kujikwamua.
Bodaboda serikali
imewatambua na imewathamini ni juu yenu kutii ili mpate kuondokana na adha ya
kukimbizana na Polisi sambamaba na kuondokana na Umaskini.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
Post A Comment: