Joseph Mgile akiwa ameweka pozi la kupigwa picha na waandishi baada ya kamera kumzonga zonga.
Taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa (takukuru) Mkoani Geita
imemfikisha mahamani mfanyakazi wa mgodi wa kuchimba dhahabu GGM
Joseph Mgile kwa kosa la
kuomba ruswa ya ngono wakati wa kutoa ajira ndani ya mgodi huo.
Wakisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama
ya wilaya ya Geita Ushindi Swaro wanasheria wa takukuru Kelvin Murusuri
akishilikiana na Felister Chamba wameiambia mahakama hiyo kuwa tarehe moja juni
mwa mwaka 2015 Joseph Mgile akiwa afisa
mwajiri wa mgodi wa GGM aliomba ruswa ya ngono kutoka kwa Saida Honga
kwa ajiri ya kumpatia kazi.
Wanasheria hao wamendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa pamoja na Saida
kuwa na vigezo vyote vya kupata kazi na kushinda kwenye kazi alizoziomba ni
engineering,infrastructure,data process clack, lakini alishindwa kupata kazi
kwa kigezo cha kukataa kutoa rushwa ya ngono.
Mara baada ya kumaliza kusoma shitaka hilo mshitakiwa alikana
shitaka hilo na kuomba kupatiwa dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini
wawili na kila mmoja kusaini hati ya milioni saba kila mmoja.
Mshitakiwa huyo amekosa vigezo vya dhamana na kupelekwa rumande na
kesi hiyo inatajiwa kuanza kusikilizwa kesho.
Post A Comment: