Wamelalamikia kuhusu namna wanavyoshambuliwa na kupokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wanasiasa na umma.
Waandishi wa habari nchini Kenya wameandamana hii leo kupinga kile wanachosema ni K kuongezeka kwa "mazingira hatarishi ya kazi".
Maandamano hayo yaliyofanyika jijini Nairobi yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari yanakuja siku kadhaa baada ya mwandishi wa habari za kisiasa kufa katika mazingira ya kutatanisha eneo la kilifi pwani ya Kenya.
Katika waraka wao walioutuma kwa bunge waandishi hao walilalamika kuhusu namna wanavyoshambaliwa na kupokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wanasiasa na umma.
Wanahabari wamesisitiza kuwa wanayo haki ya kikatiba ya kutangaza taarifa.
Wamesema baadhi ya viongozi wa kisiasa wa serikali kuu, kaunti pamoja na raia wamekuwa wakijiamulia wenyewe kuchukua sheria mkononi kuidhinisha mateso na kuwashambulia waandishi wa habari kwa kuwapiga na kuwatusi kwenye mitandao ya kijamii na baadhi yao kuwatishia mauaji ikiwa hawatatoa taarifa zinazowapendelea.
Wamesisitiza kuwa wanayo haki ya kikatiba ya kutangaza taarifa.
Waandishi wa habari watano wamekwishauwawa nchini Kenya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita
Taarifa yao imeongeza kuwa visa hivi dhidi ya waandishi wa habari huenda ni njama za wadau wa serikali na watu binafsi za kutaka kudhibiti juhudi za waandishi wa habari wanaoripoti taarifa kuhusu , haki za jamii, wizi wa ardhi na ufisadi zififie.
Waandishi wa habari watano wameuawa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita nchini Kenya.
Post A Comment: