![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati na ulinzi akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya Mkoa huo. |
Na,Joel Maduka,Geita
Imeelezwa
kuwa vifo vinavyotokana na wivu wa Mapenzi vimekuwa vikichangia kurudisha nyuma
maendeleo ya mkoa wa Geita kwa kuwa vinapoteza nguvu kazi ya taifa.
Mkuu wa mkoa
wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi alisema vifo hiyo vinachangia kurudisha nyuma
maendeleo ya mkoa huo kutokana na wengi wao kujichukulia maamuzi ya haraka bila
kuwashirikisha baadhi ya watu wanaoweza kuwasaidia kutatua migogoro yao.
Ameyataja
baadhi ya matukio makubwa yaliyosababisha watu kufariki katika maeneo mengi ya
mkoa huo kuwa ni kujichukulia sheria mkononi, ugomvi wa kuwania mali,
ushirikina na wivu wa mapenzi.
Mhandisi
Luhumbi ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini kuwashauri na kuwasaidia
watu wenye migogoro ya kifamilia ili kuendelea kuuweka mkoa huo katika hali ya
usalama
Post A Comment: